Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 29. Ni mwisho gani wenye msiba utakaolipata shamba la mizabibu la Yehova la Israeli?

      29 Isaya amalizia ujumbe huo wa unabii kwa kusimulia mwisho wenye msiba kwa wale ambao “wameikataa sheria ya BWANA” na kushindwa kuzaa matunda ya uadilifu. (Isaya 5:24, 25; Hosea 9:16; Malaki 4:1) Atangaza hivi: “[Yehova] atawatwekea bendera mataifa toka mbali, naye atawapigia miunzi tokea mwisho wa nchi; na tazama, watakuja mbio mbio upesi sana.”—Isaya 5:26; Kumbukumbu la Torati 28:49; Yeremia 5:15.

      30. Ni nani atakayekusanya “taifa kubwa” dhidi ya watu wa Yehova, na matokeo yatakuwaje?

      30 Nyakati za kale, mhimili uliokuwa mahali palipoinuka ungalikuwa kama “bendera [“ishara,” NW],” au kama mahali pa kukusanyika, kwa watu au majeshi. (Linganisha Isaya 18:3; Yeremia 51:27.) Sasa Yehova mwenyewe atakusanya “mataifa [“taifa kubwa,” NW]” ili litekeleze hukumu yake.b ‘Atalipigia miunzi,’ yaani, atageuza fikira za taifa hilo kwa watu wake waliopotoka ambao ni kama chombo kinachostahili kutekwa. Kisha nabii huyo afafanua shambulio la kasi na lenye kutisha la washindi hao walio kama simba ambao ‘watakamata mateka,’ yaani, taifa la Mungu, na “kuyachukua na kwenda zao salama” utekwani. (Soma Isaya 5:27-30a.) Na tokeo kwa nchi ya watu wa Yehova lahuzunisha kama nini! “Mtu akiitazama nchi, ataona giza na dhiki nayo nuru imetiwa giza katika mawingu yake.”—Isaya 5:30b.

  • Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • b Katika unabii mwingine mbalimbali, Isaya atambulisha Babiloni kuwa taifa linalotekeleza hukumu ya Yehova yenye kuangamiza dhidi ya Yuda.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki