-
Unafiki Wafichuliwa!Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
17. Yehova anawasihije watu wake wazitii sheria za Sabato?
17 Sabato ilikuwa wonyesho wa jinsi ambavyo Mungu huhangaikia sana masilahi ya kimwili na ya kiroho ya watu wake. Yesu alisema hivi: “Sabato ilikuja kuwako kwa ajili ya binadamu.” (Marko 2:27) Siku hiyo iliyotakaswa na Yehova iliwapa Waisraeli nafasi ya pekee ya kuonyesha kwamba wanampenda Mungu. Kwa kuhuzunisha, kufikia wakati wa Isaya siku hiyo imekwisha zorota ikawa ya kufuata desturi tupu na kujihusisha katika tamaa za ubinafsi. Basi, kwa mara nyingine Yehova ana sababu nzuri ya kuwashutumu vikali watu wake. Na kwa mara nyingine tena, anajaribu kuifikia mioyo yao. Anasema hivi: “Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika BWANA; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo.”—Isaya 58:13, 14.
-
-
Unafiki Wafichuliwa!Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
19. Ikiwa watu wa Mungu watageuka waanze kushika Sabato, watapata baraka zipi?
19 Na bado, Wayahudi wakijifunza kutokana na nidhamu hiyo kisha wageuke na kuanza kuuheshimu mpango wa Sabato, watapata baraka nyingi. Matokeo mema ya kufuata ibada ya kweli na kuiheshimu Sabato yatafurika yaenee katika sehemu zote za maisha yao. (Kumbukumbu la Torati 28:1-13; Zaburi 19:7-11) Kwa mfano, Yehova atawafanya watu wake ‘wapande mahali pa nchi palipoinuka.’ Usemi huo unamaanisha kupata usalama na kuwashinda maadui. Yule anayefaulu kusimamia mahali palipoinuka, yaani vilima na milima, ndiye anayefaulu kuisimamia nchi. (Kumbukumbu la Torati 32:13; 33:29) Wakati mmoja Israeli walimtii Yehova, na taifa hilo lilifurahia ulinzi wake na kuheshimiwa, hata kuogopwa, na mataifa mengine. (Yoshua 2:9-11; 1 Wafalme 4:20, 21) Wakimgeukia Yehova tena kwa kumtii, watarudishiwa kiasi fulani cha utukufu huo wa zamani. Yehova atawapa watu wake sehemu kamili ya “urithi wa Yakobo,” yaani zile baraka zilizoahidiwa kupitia agano Lake na baba zao wa zamani, na hasa baraka ya kumiliki Nchi ya Ahadi bila wasiwasi wowote.—Zaburi 105:8-11.
-