Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wale Wanaotembea Katika Nuru Hushangilia
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Machi 1
    • 2 Tunapozingatia hilo, tunaweza kuelewa uzito wa hali inayofafanuliwa na nabii Isaya. Alisema hivi: “Tazama, giza litaifunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu.” (Isaya 60:2) Ni wazi kwamba giza hilo si giza halisi. Isaya hakumaanisha kwamba siku fulani jua, mwezi, na nyota zitaacha kuangaza. (Zaburi 89:36, 37; 136:7-9) Badala yake, alikuwa akizungumzia giza la kiroho. Lakini giza la kiroho laweza kusababisha kifo. Hatuwezi kuishi bila nuru ya kiroho kwa muda mrefu kama vile tusivyoweza kuishi bila nuru halisi.—Luka 1:79.

      3. Kwa kuzingatia maneno ya Isaya, Wakristo wapaswa kufanya nini?

      3 Kwa kuzingatia hilo, ni jambo muhimu kutambua kwamba ijapokuwa maneno ya Isaya yalitimizwa katika Yuda la kale, yanatimizwa kwa kiwango kikubwa zaidi leo. Naam, katika wakati wetu ulimwengu umefunikwa na giza la kiroho. Katika hali hiyo hatari, nuru ya kiroho ni muhimu kuliko mambo yote. Ndiyo sababu inafaa Wakristo watii himizo hili la Yesu: “Acheni nuru yenu ing’ae mbele ya watu.” (Mathayo 5:16) Wakristo waaminifu wanaweza kuwaangazia nuru wapole walio katika giza, na hivyo kuwapa fursa ya kupata uhai.—Yohana 8:12.

  • Wale Wanaotembea Katika Nuru Hushangilia
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Machi 1
    • 4. Maneno ya kiunabii ya Isaya yalitimizwa lini mara ya kwanza, lakini tayari kulikuwa na hali gani katika siku zake?

      4 Maneno ya Isaya kuhusu jinsi ambavyo giza lingeifunika dunia yalitimizwa mara ya kwanza Yuda lilipofanywa ukiwa na watu wake walipokuwa katika utekwa Babiloni. Hata hivyo, hata kabla ya wakati huo, katika siku za Isaya mwenyewe, tayari sehemu kubwa ya taifa hilo ilikuwa imefunikwa na giza la kiroho, jambo lililomchochea awasihi hivi watu wa nchi yake: “Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni twende katika nuru ya BWANA”!—Isaya 2:5; 5:20.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki