-
Wachukuaji Nuru—Kwa Kusudi Gani?Mnara wa Mlinzi—1993 | Januari 15
-
-
16, 17. Yehova aliangazaje utukufu wake juu ya tengenezo lake lililo kama mwanamke katika 1914, na alimpa amri gani?
16 Kwa maneno yenye kuchochea moyo, Maandiko yanasimulia njia ambayo nuru ya kimungu inaenezwa kwa watu kila mahali. Isaya 60:1-3 linaloelekezwa kwa “mwanamke” wa Yehova au tengenezo lake la kimbingu la watumishi waaminifu-washikamanifu husema hivi: “Ondoka, [Ee mwanamke, NW] uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa BWANA [Yehova, NW] umekuzukia. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu; bali BWANA [Yehova, NW] atakuzukia wewe, na utukufu wake utaonekana juu yako. Na mataifa wataijilia nuru yako, na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.”
-
-
Wachukuaji Nuru—Kwa Kusudi Gani?Mnara wa Mlinzi—1993 | Januari 15
-
-
18. (a) Kwa nini giza laifunika dunia, kama ilivyotabiriwa kwenye Isaya 60:2? (b) Watu mmoja mmoja wanaweza kukombolewaje kutoka katika giza la dunia?
18 Kinyume cha hayo, giza laifunika dunia na giza kuu lafunika vikundi vya kitaifa. Kwa nini? Kwa sababu mataifa yanakataa serikali ya Mwana mpendwa wa Mungu kwa kupendelea utawala wa kibinadamu. Wanafikiri kwamba kwa kuondolea mbali namna moja ya serikali ya kibinadamu na kukubali nyingine, wataweza kusuluhisha matatizo yao. Lakini hilo halileti kitulizo wanachotumainia. Wanashindwa kuona ni nani kutoka makao ya roho anayeyaongoza mataifa bila kuonekana. (2 Wakorintho 4:4) Wanakataa Chanzo cha nuru ya kweli na hivyo wamo gizani. (Waefeso 6:12) Hata hivyo, bila kujali yale yanayofanywa na mataifa, watu mmoja mmoja wanaweza kukombolewa kutoka katika giza hilo. Kwa njia gani? Kwa kuwa na imani kamili katika Ufalme wa Mungu na kujitiisha chini yao.
19, 20. (a) Kwa nini na kwa jinsi gani utukufu wa Yehova umewaangazia wafuasi wa Yesu wapakwa-mafuta? (b) Yehova amewafanya wapakwa-mafuta wake wawe wachukuaji nuru kwa kusudi gani? (c) Kama ilivyotabiriwa, “wafalme” na “mataifa” wamevutwaje kwenye nuru ya kupewa na Mungu?
19 Jumuiya ya Wakristo haijazoeza imani katika Ufalme wa Mungu na haijajitiisha chini yao. Lakini wafuasi wapakwa-mafuta wa Yesu Kristo wamefanya hivyo. Kama tokeo, nuru ya Yehova ya kibali cha kimungu imeangaza juu ya wawakilishi hao wenye kuonekana wa mwanamke wake wa kimbingu, na utukufu wake umedhihirika kwao. (Isaya 60:19-21) Wao huonea shangwe nuru ya kiroho ambayo hakuna badiliko lolote katika mandhari ya kisiasa au ya kiuchumi ya ulimwengu linaloweza kuwanyang’anya. Wao wameona Yehova akiwakomboa kutoka Babuloni Mkubwa. (Ufunuo 18:4) Wanaonea shangwe tabasamu ya kibali chake kwa sababu wamekubali nidhamu yake na wametegemeza enzi kuu yake kwa uaminifu-mshikamanifu. Wao wana mataraja mazuri ya wakati ujao, na wanashangilia katika tumaini ambalo ameweka mbele yao.
-