Kama Njiwa Warukao Kwenda Kwenye Nyumba Zao
NJIWA labda walikuwa miongoni mwa ndege wa kwanza kufugwa na mwanadamu. Maelfu ya miaka iliyopita, Wamisri—wakitaka kuwa na ugavi wa chakula wa mwaka mzima—waliwajengea nyumba karibu na makao yao. Nyama ya ndege hao ilithaminiwa sana, na kinyesi chao kilitumiwa kuwa mbolea. Kufikia Enzi za Kati, nyumba za njiwa zilitamaniwa sana hivi kwamba katika nchi nyinginezo watu wakuu au viongozi wa dini tu ndio walioruhusiwa kuwa nazo.
Ingawa kuku wamechukua mahali pa njiwa kuwa vyanzo vya nyama katika nyumba nyingi, baadhi ya nyumba za njiwa za kale zaweza kupatikana. Nyumba za njiwa zinazoonyeshwa hapa hupatikana katika Misri.
Wakirudi jioni kwa wingi, wingu halisi la ndege hao hushuka kwenye nyumba ya njiwa. Nabii Mwebrania Isaya alirejezea hilo alipouliza hivi: “Ni nani hawa warukao kama wingu, na kama njiwa waendao madirishani kwao?” Kama vile tafsiri nyingine husema: “Ni nani hawa waabirio kama mawingu, warukao kama njiwa waendao kwenye nyumba zao?”—Isaya 60:8; The New English Bible.
Jibu lapatikana leo katika mamia ya maelfu ya watu wenye kumhofu Mungu wanaomiminika kwenye tengenezo la Yehova. Katika Majumba ya Ufalme ya Mashahidi wa Yehova, wanajifunza kuwa na tumaini katika Mungu. (Isaya 60:9) Miongoni mwa watu wa Mungu, wao wanagundua kwamba thamani za kiroho, imani iliyo hai, na ushirika ufaao hutoa hisi ya amani na usalama unaofanana na ule unaopatikana na njiwa katika nyumba yake.
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]
Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.