Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Paradiso Iliyorudishwa Yamtukuza Mungu
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Agosti 15
    • 1, 2. (a) Kupitia mnabii wake Isaya, Mungu alitabiri nini kuhusu dunia? (b) Tunapotazama miaka elfu moja ndani ya wakati ujao, twaona nini?

      YEHOVA aliiumba dunia iwe sayari iliyo chini ya nyayo zake, iwe kibago cha ufananisho cha kuwekea nyayo zake. Kupitia Isaya mnabii wake, Mungu alitabiri kwamba yeye ‘angepatukuza mahali penyewe pa nyayo zake.’ (Isaya 60:13, NW) Kwa msaada wa Biblia iliyovuviwa, twaweza kutazama, kana kwamba kwa darubini yenye nguvu nyingi, miaka elfu moja ndani ya wakati ujao wa kibinadamu. Macho yetu yakabiliana na muono wenye uvutio wa kupindukia! Dunia nzima yang’aa kwa upendezi wa ajabu uliotokezwa na Mtunza-bustani aliye mkubwa wa wote katika ulimwengu wote mzima. Wakati huo aina ya binadamu itakuwa imerudishiwa Paradiso duniani pote!

  • Paradiso Iliyorudishwa Yamtukuza Mungu
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Agosti 15
    • 3, 4. (a) Mbingu na dunia zitalinganaje? (b) Malaika wataitikiaje Paradiso irudishwapo duniani?

      3 Maelfu ya miaka kabla ya hapo, katika elezo lililovuviwa kimungu kuhusu makao yake, Mungu alinena maneno haya ya kuvutia kwa watu wake wachaguliwa: “Mbingu ni kiti changu cha ufalme, na dunia ni kibago cha kuwekea nyayo zangu.” (Isaya 66:1, NW) Utukufu wenyewe tu wa “kibago cha kuwekea nyayo” zake, ile dunia-Paradiso, wapasa ufaane na utukufu wa kiti chake cha enzi katika vile vimo vya juu visivyoonekana.

  • Paradiso Iliyorudishwa Yamtukuza Mungu
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Agosti 15
    • 6. Baada ya Har–Magedoni, dunia itajazwaje wakaaji?

      6 Ingawa waokokaji wa Har–Magedoni watakuwa wachache kwa ulinganisho, dunia haitajazwa watu kikamili kwa kuzaa watoto tu kwa upande wao. Yehova ‘atapatukuza pia mahali pa nyayo zake’ kwa kuwarudisha kwenye uhai wale walio katika makaburi ya ukumbusho ambao waja chini ya manufaa za dhabihu ya ukombozi ya Kristo. Hao, nao, watakuwa na pendeleo la kuishiriki kazi yenye upendezi tele ya kugeuza tufe letu la kidunia liwe paradiso yenye uzuri uzidio chochote kile.—Matendo 24:15.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki