Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ‘Mkashangilie Daima kwa Ajili ya Hivi Niviumbavyo’
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 7, 8. Watu wa Yehova walio na vichwa vigumu wamechocheaje hasira yake?

      7 Wayahudi wenye vichwa vigumu wamechochea hasira ya Yehova mara nyingi kwa mwenendo wao wa aibu. Yehova anaeleza hivi kuhusu matendo yao yenye kuudhi: “Watu wanikasirishao mbele za uso wangu daima, wakitoa dhabihu katika bustani zao, na kufukiza uvumba juu ya matofali; waketio kati ya makaburi, na kulala katika mahali pao pa siri; walao nyama ya nguruwe, na mchuzi wa vitu vinichukizavyo u katika vyombo vyao; watu wasemao, Simama peke yako, usinikaribie mimi, kwa maana mimi ni mtakatifu kuliko wewe; watu hao ni moshi puani mwangu, moto uwakao mchana kutwa.” (Isaya 65:3-5) Watu hawa ambao wanaonekana kama wenye kicho wanamwudhi Yehova ‘mbele za uso wake’—usemi unaoweza kumaanisha ujeuri na madharau. Hawajitahidi hata kidogo kuyaficha machukizo yao. Je, si kweli kwamba hatia ya dhambi zao inazidi kuwa kubwa kwa sababu wanazitenda pale pale mbele za Yule wanayepaswa kumheshimu na kumtii?

      8 Kwa kweli, watenda-dhambi hao wanaojiona kuwa waadilifu ni kama wanawaambia hivi Wayahudi wenzao: ‘Kaa mbali nami, kwa sababu mimi ni mtakatifu kukushinda.’ Unafiki gani huo! Watu hao wanaodai eti ni “wenye kicho” wanatoa dhabihu na kuiwashia uvumba miungu ya uwongo, jambo linalokatazwa na Sheria ya Mungu. (Kutoka 20:2-6) Wameketi kati ya makaburi,hiyo ikiwafanya wawe wachafu kulingana na Sheria.(Hesabu 19:14-16)Wanakula nyama ya nguruwe, chakula kichafu.a (Mambo ya Walawi 11:7) Hata hivyo, utendaji wao wa kidini unawafanya wajione kuwa watakatifu kuliko Wayahudi wengine, na wanataka wengine wakae mbali nao, eti watu hao wasitakasike au kuwa safi kwa sababu ya kushirikiana nao. Hata hivyo, jambo hilo halipatani hata kidogo na maoni ya yule Mungu ambaye hutaka apewe “ujitoaji wa pekee”!—Kumbukumbu la Torati 4:24, NW.

  • ‘Mkashangilie Daima kwa Ajili ya Hivi Niviumbavyo’
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • a Watu wengi wanafikiri kwamba watenda dhambi hawa walikuwa kati ya makaburi wakijaribu kuwasiliana na wafu. Kula kwao nyama ya nguruwe huenda kukawa kulihusiana na ibada ya sanamu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki