-
Je, Utakuwepo Katika Ulimwengu Mpya?Mnara wa Mlinzi—2000 | Aprili 15
-
-
14, 15. Ni utendaji gani wenye kuthawabisha uwezao kutarajia kulingana na Isaya 65:21, 22?
14 Badala ya kuzungumzia sana jinsi mtenda-dhambi wa kukusudia awezavyo kuondolewa, Isaya afafanua hali za maisha zitakazokuwapo katika ulimwengu mpya. Jiwazie ukiwa katika hali hizo. Huenda mambo uwezayo kuwazia kwanza yakawa yale unayopenda sana. Isaya azungumzia mambo hayo katika mstari wa 21 na 22: “Watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake. Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine; maana kama siku za mti ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi.”
-
-
Je, Utakuwepo Katika Ulimwengu Mpya?Mnara wa Mlinzi—2000 | Aprili 15
-
-
16. Kwa nini unaweza kutarajia ulimwengu mpya uwe wenye kuridhisha daima?
16 Jambo la maana zaidi kuliko kujua mambo hayo madogo-madogo ni kwamba utakuwa na makao yako mwenyewe. Yatakuwa yako—si kama vile leo uwezavyo kujitahidi kujenga kisha mtu mwingine akanufaika. Isaya 65:21 pia lasema kwamba utapanda na kula matunda. Ni wazi kwamba hilo laonyesha jinsi hali itakavyokuwa kwa ujumla. Utaridhishwa sana na jitihada zako, matokeo ya jasho lako mwenyewe. Nawe utaweza kufanya hivyo kwa muda mrefu—“kama siku za mti.” Bila shaka hilo lapatana na ufafanuzi wa “vitu vyote kuwa vipya”!—Zaburi 92:12-14.
-