Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wokovu na Kushangilia Chini ya Utawala wa Mesiya
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 6. Yatabiriwa kwamba Mesiya atakuwa mtawala wa aina gani?

      6 Mesiya atakuwa mtawala wa aina gani? Je, atakuwa kama Mwashuri mkatili, mshupavu, anayeharibu ufalme wa kaskazini wa Israeli wenye makabila kumi? Sivyo hata kidogo. Isaya asema hivi kumhusu Mesiya: “Roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA; na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA.” (Isaya 11:2, 3a) Mesiya ateuliwa na roho takatifu ya Mungu, wala si kwa kutiwa mafuta. Jambo hilo latukia kwenye ubatizo wa Yesu, Yohana Mbatizaji aonapo roho takatifu ya Mungu iliyo kama njiwa ikiteremka juu ya Yesu. (Luka 3:22) Roho ya Yehova ‘yakaa juu ya’ Yesu, naye atoa uthibitisho wa jambo hilo atendapo kwa hekima, ufahamu, shauri, uweza, na ujuzi. Ni sifa bora kama nini anazostahili mtawala kuwa nazo!

  • Wokovu na Kushangilia Chini ya Utawala wa Mesiya
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 8. Yesu apataje furaha katika kumcha Yehova?

      8 Mesiya anamchaje Yehova? Kwa hakika, Yesu hatishwi na Mungu, akihofu hukumu yake. Badala yake, Mesiya anamcha Mungu kwa staha, staha yenye upendo kwake. Mtu mwenye kumhofu Mungu hutamani ‘kufanya sikuzote mambo yale yanayompendeza,’ kama afanyavyo Yesu. (Yohana 8:29) Kwa neno na tendo, Yesu afundisha kwamba hakuna shangwe kubwa zaidi kuliko ile inayotokana na kutembea kila siku katika hofu ifaayo ya Yehova.

      Hakimu Mwadilifu na Mwenye Rehema

      9. Yesu atoa kielelezo gani kwa wale wenye wajibu wa kuamua mambo katika kutaniko la Kikristo?

      9 Isaya atabiri sifa zaidi za Mesiya: “Hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake.” (Isaya 11:3b) Iwapo ungefikishwa mahakamani, je, hungefurahia hakimu kama huyo? Akiwa katika cheo chake cha Hakimu wa wanadamu wote, Mesiya hapeperushwi na hoja zisizo za kweli, hila za mahakamani, porojo, au mambo ya kijuujuu, kama vile mali. Yeye atambua udanganyifu naye aona mengi zaidi kuliko sura ya nje inayopotosha, huku akitambua “mtu wa siri wa moyoni,” “mtu aliyefichika.” (1 Petro 3:4, NW, kielezi-chini) Kielelezo bora zaidi cha Yesu ni kigezo kwa wote wenye wajibu wa kuamua mambo katika kutaniko la Kikristo.—1 Wakorintho 6:1-4.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki