Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kumjua Mungu wa Kweli—Kwamaanisha Nini?
    Je! Ulimwengu Usio na Vita Utakuwako Wakati Wowote?
    • 7 Lakini namna gani ile hoja ya kwamba jina la Mungu ni “takatifu mno kuweza kutamkwa?” Basi, je, haielekei kuwa jambo la akili kwamba kama Mungu aliona jina lake kuwa takatifu mno kwa wanadamu kuweza kulitamka, hangalilifunua kabisa? Uhakika wa kwamba katika maandishi ya awali ya Maandiko ya Kiebrania, jina la Mungu la kibinafsi huonekana mara zaidi ya 6,800, huonyesha kwamba yeye hutaka watu wamjue na kutumia jina lake. Tofauti sana na kuwekea mipaka utumizi wa jina lake ili kuzuia lisitendewe kwa njia isiyo ya staha, Mungu hutia moyo kwa kurudia-rudia na hata huwaamuru watu wake watumie jina lake na kulijulisha. Kufanya hivyo kulikuwa uthibitisho wa uhusiano wao wa karibu pamoja naye na pia upendo wao kwake. (Zaburi 91:14) Nabii Isaya, alionyesha waziwazi ni nini yaliyo mapenzi ya Mungu kuhusu jambo hilo wakati alipotaarifu hivi: “Sifuni BWANA [Kiebrania, יהזה=YHWH=Yehova], pigeni mbiu ya jina Lake. Fanyeni matendo yake yajulikane miongoni mwa vikundi vya watu; julisheni kwamba jina Lake limetukuka.”—Isaya 12:4. Ona pia Mika 4:5; Malaki 3:16; Zaburi 79:6; 105:1; Mithali 18:10.

  • Kumjua Mungu wa Kweli—Kwamaanisha Nini?
    Je! Ulimwengu Usio na Vita Utakuwako Wakati Wowote?
    • “Sifuni BWANA [יהזה], pigeni mbiu ya jina Lake. Fanyeni matendo yake yajulikane miongoni mwa vikundi vya watu; julisheni kwamba jina Lake limetukuka.”d—Isaya 12:4, italiki ni zetu; Zaburi 105:1.

  • Kumjua Mungu wa Kweli—Kwamaanisha Nini?
    Je! Ulimwengu Usio na Vita Utakuwako Wakati Wowote?
    • d Fungu hili la maneno “pigeni mbiu ya jina Lake” (Kiebrania, קראו בשמו) laweza kutafsiriwa pia “mwiteni kwa jina lake.” (Linganisha The New English Bible.) Mtungo uo huo wa Kiebrania unapatikana kwenye Mwanzo 12:8, ambapo hutafsiriwa na Tanakh: “[Abram] aliita BWANA kwa jina.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki