-
Shauri la Yehova Dhidi ya MataifaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
25. Ni nini linalotukia juu ya Misri ya kale kwa utimizo wa Isaya 19:1-11?
25 Jirani wa karibu zaidi wa Yuda upande wa kusini ni Misri, adui wa muda mrefu wa watu wa agano wa Mungu. Isaya sura ya 19 yasimulia hali zenye vurugu nchini Misri wakati wa maisha ya Isaya. Kuna vita ya wenyewe kwa wenyewe Misri, kukiwa vita ya “mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme.” (Isaya 19:2, 13, 14) Wanahistoria watoa uthibitisho unaohusu nasaba za wafalme zenye kupambana zikitawala sehemu mbalimbali za nchi hiyo kwa wakati mmoja. Hekima wanayojivunia Wamisri, pamoja na ‘sanamu zao, na waganga wao,’ haiwaokoi kutoka katika “mikono ya bwana mgumu.” (Isaya 19:3, 4) Ashuru, Babiloni, Uajemi, Ugiriki, na Roma, zaishinda Misri kabisa. Matukio hayo yote yatimiza unabii mbalimbali wa Isaya 19:1-11.
-
-
Shauri la Yehova Dhidi ya MataifaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
28. Katika siku ya hukumu, dini isiyo ya kweli itaweza kufanya nini ili kuuokoa mfumo huu wa mambo?
28 “Roho ya Misri itamwagika kabisa katikati yake, nami nitayabatilisha mashauri yake, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli, na kwa wachawi.” (Isaya 19:3) Musa alipoenda mbele ya Farao, makuhani wa Misri waliaibishwa, kwa kuwa hawakuweza kulingana na Yehova katika nguvu. (Kutoka 8:18, 19; Matendo 13:8; 2 Timotheo 3:8) Vivyo hivyo, katika siku ya hukumu, dini isiyo ya kweli haitaweza kuuokoa mfumo huu wenye ufisadi. (Linganisha Isaya 47:1, 11-13.) Hatimaye, Misri ikaja chini ya “bwana mgumu,” Ashuru. (Isaya 19:4) Hilo laonyesha kimbele wakati wenye huzuni unaokabili mfumo huu wa mambo.
-