Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Amani Ile ya Uhalisi
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Desemba 15
    • “[2] Na lazima itukie katika sehemu ya mwisho ya zile siku kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utakuwa wenye kuthibitishwa imara juu ya kileleta cha milima, nao kwa uhakika utainuliwa juu ya vilima; na ni lazima mataifa yote yamiminike kuuendea. [3] Na vikundi vingi vya watu kwa uhakika vitaenda na kusema: ‘Njoni, nyinyi watu, na acheni twende juu kwenye mlima wa Yehova, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo; na yeye atatuagiza kuhusu njia zake, na sisi tutatembea katika vijia vyake.’ Kwa maana kutoka Sayuni sheria itatokeza mbele, na neno la Yehova kutoka Yerusalemu. [4] Na yeye kwa uhakika atatoa hukumu miongoni mwa mataifa na kunyoosha mambo kwa habari ya vikundi vingi vya watu. Na wao watalazimika kufua panga zao ziwe plau za kulimia na mikuki yao iwe makasi ya kupogolea. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa, wala hawatajifunza vita tena.“

  • Amani Ile ya Uhalisi
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Desemba 15
    • Namna gani leo? Angalia kwamba Isaya atanguliza dibaji ya ujumbe wake kwa taarifa hii: “Ni lazima itukie katika sehemu ya mwisho ya zile siku.” Tafsiri nyinginezo husema: “Katika siku za mwisho.” (Union Version) Ushuhuda hutokezwa kwa ukawaida katika kurasa za gazeti hili kuunga mkono jambo la kwamba tumekuwa tukiishi katika siku za mwisho za taratibu hii ya sasa ya mambo ya ulimwengu tangu 1914. Kwa hiyo, yatupasa tutarajie kuona nini, kulingana na mistari ya 3 na 4?

  • Amani Ile ya Uhalisi
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Desemba 15
    • Nabii ataarifu kwamba “mlima wa nyumba ya Yehova utakuwa wenye kuthibitishwa imara juu ya kileleta cha milima” na “utainuliwa juu ya vilima.” Nyakati za kale, milima na vilima fulani vilitumika kuwa nyanja za ibada ya sanamu na maabadi matakatifu ya miungu bandia. Mfalme Daudi alipoleta lile Sanduku takatifu kwenye hema alilokuwa amepiga juu ya Mlima Sayuni (Yerusalemu), meta 760 hivi juu ya usawa wa bahari, kwa uwazi yeye alikuwa akitenda kupatana na mwelekezo wa kimungu. Baadaye, wakati lile hekalu kubwa la Yehova lilipojengwa juu ya Mlima Moria, mtajo “Sayuni” ukaja kuhusisha ndani uwanja wa hekalu, kwa hiyo hekalu lilikuwa na mwinuko ulio juu kuliko baadhi ya mahali-mahali pa kipagani palipolizunguka. Yerusalemu lenyewe liliitwa pia “mlima mtakatifu” wake; hivyo, ibada ya Yehova ilibaki katika cheo kilichokwezwa. —Isaya 8:18; 66:20.

      Kwa hiyo leo, ibada ya Yehova Mungu imekuwa yenye kuinuka kama mlima wa ufananisho. Imeinuka juu kwa umashuhuri kwa njia yenye kuonekana na wote, kwa maana imefanya jambo ambalo hakuna dini nyingine imeweza kulifanya. Jambo gani hilo? Imeungamanisha vizuri waabudu wote wa Yehova, ambao wameterema kufua panga zao zikawa plau za kulimia na hawajifunzi vita tena. Vizuizi vya kitaifa na vya rangi haviwagawanyi tena. Wao huishi wakiwa kikundi cha watu walioungamana, udugu mmoja, hata ingawa wametapakaa sehemu zote za mataifa ya ulimwengu.—Zaburi 33:12.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki