Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Amani Ile ya Uhalisi
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Desemba 15
    • “[2] Na lazima itukie katika sehemu ya mwisho ya zile siku kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utakuwa wenye kuthibitishwa imara juu ya kileleta cha milima, nao kwa uhakika utainuliwa juu ya vilima; na ni lazima mataifa yote yamiminike kuuendea. [3] Na vikundi vingi vya watu kwa uhakika vitaenda na kusema: ‘Njoni, nyinyi watu, na acheni twende juu kwenye mlima wa Yehova, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo; na yeye atatuagiza kuhusu njia zake, na sisi tutatembea katika vijia vyake.’ Kwa maana kutoka Sayuni sheria itatokeza mbele, na neno la Yehova kutoka Yerusalemu. [4] Na yeye kwa uhakika atatoa hukumu miongoni mwa mataifa na kunyoosha mambo kwa habari ya vikundi vingi vya watu. Na wao watalazimika kufua panga zao ziwe plau za kulimia na mikuki yao iwe makasi ya kupogolea. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa, wala hawatajifunza vita tena.“

      Kwanza, ni lazima sisi tukiri kwamba Muumba wetu, Yehova, ana haki ya kutuagiza “kuhusu njia zake,“ambazo, kama vile Isaya alivyoandika baadaye, ziko ‘juu kuliko njia zetu.’ (Isaya 55:9) Watu wengi, hasa viongozi wa ulimwengu wenye kujihesabu wenyewe kuwa mashuhuri, huona ikiwa vigumu kukiri hivyo. Njia zao wenyewe ndizo tu zilizo sawa machoni pao wenyewe. Na bado, uhakika wa kwamba njia zao hazijaongoza kwenye amani ya ulimwengu wala kwenye ondoleo la silaha zaonyesha kwa uhakika kwamba ni ubatili kuendelea kufuatia mwendo huo.

      Pili, angalia tamaa yenye hamu nyingi ya watu mmoja mmoja kujipatanisha na sheria za Mungu: “Sisi tutatembea katika vijia vyake.“Ni kwa msingi huo tu kwamba panga zitafuliwa ziwe plau za kulimia na mikuki iwe makasi ya kupogolea duniani pote. Ni jinsi gani mradi huo wenye kutamaniwa sana waweza kuja kufikiliwa?

      Maagizo ya Kimungu

      Watu wengi wana nakala ya Biblia, kile kitabu kilicho na maagizo ya Yehova Mungu, lakini mengi zaidi yatakwa kuliko kuwa nacho tu. Isaya asema kwamba sheria na maneno ya Yehova yatokana na “Yerusalemu.“Hiyo yamaanisha nini? Katika siku ya Isaya, lile jiji halisi lilikuwa ndicho chanzo cha mamlaka ya kifalme iliyotegemewa na Waisraeli wote waaminifu. (Isaya 60:14) Baadaye, wakati wa mitume wa Yesu Kristo, Yerusalemu palikuwa pangali ndipo mahali pakuu pa maagizo yenye kutoka kwa baraza lenye kuongoza la Kikristo lililokuwa katika jiji hilo.—Matendo 15:2; 16:4.

  • Amani Ile ya Uhalisi
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Desemba 15
    • Nabii ataarifu kwamba “mlima wa nyumba ya Yehova utakuwa wenye kuthibitishwa imara juu ya kileleta cha milima” na “utainuliwa juu ya vilima.” Nyakati za kale, milima na vilima fulani vilitumika kuwa nyanja za ibada ya sanamu na maabadi matakatifu ya miungu bandia. Mfalme Daudi alipoleta lile Sanduku takatifu kwenye hema alilokuwa amepiga juu ya Mlima Sayuni (Yerusalemu), meta 760 hivi juu ya usawa wa bahari, kwa uwazi yeye alikuwa akitenda kupatana na mwelekezo wa kimungu. Baadaye, wakati lile hekalu kubwa la Yehova lilipojengwa juu ya Mlima Moria, mtajo “Sayuni” ukaja kuhusisha ndani uwanja wa hekalu, kwa hiyo hekalu lilikuwa na mwinuko ulio juu kuliko baadhi ya mahali-mahali pa kipagani palipolizunguka. Yerusalemu lenyewe liliitwa pia “mlima mtakatifu” wake; hivyo, ibada ya Yehova ilibaki katika cheo kilichokwezwa. —Isaya 8:18; 66:20.

      Kwa hiyo leo, ibada ya Yehova Mungu imekuwa yenye kuinuka kama mlima wa ufananisho. Imeinuka juu kwa umashuhuri kwa njia yenye kuonekana na wote, kwa maana imefanya jambo ambalo hakuna dini nyingine imeweza kulifanya. Jambo gani hilo? Imeungamanisha vizuri waabudu wote wa Yehova, ambao wameterema kufua panga zao zikawa plau za kulimia na hawajifunzi vita tena. Vizuizi vya kitaifa na vya rangi haviwagawanyi tena. Wao huishi wakiwa kikundi cha watu walioungamana, udugu mmoja, hata ingawa wametapakaa sehemu zote za mataifa ya ulimwengu.—Zaburi 33:12.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki