Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Isaya Atabiri ‘Tendo la Ajabu’ la Yehova
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 8. Ujumbe wa Isaya wapokewaje?

      8 Viongozi wa Yuda waitikiaje onyo la Yehova? Wamdhihaki Isaya, wakimshutumu kwamba anasema nao kama watoto: “Atamfundisha nani maarifa? atamfahamisha nani habari hii? Je! ni wale walioachishwa maziwa, walioondolewa matitini? Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo.” (Isaya 28:9, 10) Kwa maoni yao, Isaya arudia-rudia mambo kiajabu! Ayarudia-rudia maneno yake mwenyewe, akisema: ‘Yehova ameamuru hivi! Yehova ameamuru hivi! Hii ndiyo kanuni ya Yehova! Hii ndiyo kanuni ya Yehova!’a Lakini karibuni Yehova “atasema” na wakazi wa Yuda kupitia tendo fulani. Atatuma majeshi ya Babiloni dhidi yao—wageni ambao kwa kweli wanasema lugha nyingine. Pasipo shaka, majeshi hayo yatatekeleza “amri juu ya amri,” za Yehova, na Yuda itaanguka.—Soma Isaya 28:11-13.

  • Isaya Atabiri ‘Tendo la Ajabu’ la Yehova
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • a Katika Kiebrania cha awali, Isaya 28:10 ni shairi linalorudiwa-rudiwa, kama vile shairi la kusimulia watoto hadithi. Basi, viongozi wa kidini waliuona ujumbe wa Isaya kuwa wenye kurudiwa-rudiwa na wa kitoto.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki