Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sababu Mungu Aliruhusu Taabu
    Amkeni!—1991 | Juni 8
    • “Kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu. Ee BWANA [Yehova, NW], unirudi kwa haki.”—Yeremia 10:23, 24.

      MANENO hayo yaliandikwa maelfu ya miaka baada ya binadamu kuumbwa. Yeremia alitambua kwamba hadi kufikia siku yake, historia ya binadamu ilikuwa ni msiba ikilinganishwa na mwanzo mzuri ambao Mungu aliwapa wazazi wetu wa kwanza.

      Aliyoonelea Yeremia yamethibitishwa na kumbukumbu ya miaka ya ziada zaidi ya 2,500 ya historia tangu wakati wake. Msiba huo wa kibinadamu umekuwa mbaya hata zaidi. Kosa lilikuwa nini?

  • Sababu Mungu Aliruhusu Taabu
    Amkeni!—1991 | Juni 8
    • Pia kupita kwa wakati kumefunua jinsi watu waliolemewa mno na dhambi hutendeana mmoja na mwenzake. Kumekuwako vita vingi mno vyenye ukatili visivyohesabika, chuki za kikabila na kidini, kuteswa kwa wazushi, uhalifu wa aina zote wenye kutisha, na vitendo vya ubinafsi na pupa. Kuongezea hayo, umaskini na njaa vimetatiza mamilioni yasiyohesabika ya watu.

      Wakati wa maelfu ya miaka yaliyopita, ainabinadamu imejaribu kila namna ya serikali inayowazika. Hata hivyo, moja baada ya nyingine zimeshindwa kutosheleza mahitaji ya binadamu. Hivi majuzi, serikali za Ukomunisti zimekataliwa katika mabara mengi. Katika mataifa ya kidemokrasi kuna uhalifu tele, umaskini, hali ya kiuchumi isiyo imara, na ufisadi. Kweli kweli, namna zote za serikali ya kibinadamu zimethibitika kuwa zimepungukiwa.

      Zaidi ya hayo, Mungu ameruhusu wakati kwa wanadamu wafikie kilele cha ufanisi wao wa kisayansi na kimwili. Lakini je! ni maendeleo halisi wakati mahali pa uta na mshale pamechukuliwa na makombora ya nyukilia? wakati watu wanapoweza kusafiri angani lakini wasiweze kuishi pamoja duniani kwa amani? wakati mamilioni ya watu wanahofu kutoka nje usiku kwa sababu ya uhalifu?

      Jambo ambalo mtihani wa wakati huonyesha ni kwamba haiwezekani kwa binadamu ‘kuelekeza hatua zake’ kwa kufaulu kama vile isivyowezekana kwao kuishi bila chakula, maji, na hewa. Sisi tumebuniwa tutegemee Mfanyizaji wetu kwa ajili ya uongozi kama vile kwa hakika tuliumbwa tutegemee chakula, maji, na hewa.—Mathayo 4:4.

      Kwa kuruhusu uovu na taabu, Mungu ameonyesha kwa safari moja ambayo haitarudiwa tena, yale matokeo yenye kusikitisha ya kutumia vibaya hiari. Hiyo ni zawadi yenye thamani sana hivi kwamba badala ya kuwanyang’anya binadamu, Mungu amewaruhusu waone maana ya kuitumia vibaya.

      Kuhusu hiari, kichapo “Statement of Principles of Conservative Judaism” chasema hivi: “Bila ya uwezekano halisi wa watu kufanya uchaguzi mbaya wanapokabiliwa na wema na uovu, wazo lote la uchaguzi halina maana. . . . Nyingi za taabu za ulimwengu zatokana moja kwa moja na matumizi mabaya ya hiari tuliyopewa.”

      Kwa hakika, Yeremia alikuwa sahihi aliposema: “Kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.” Na Sulemani pia alikuwa sahihi aliposema hivi: “Mtu mmoja ana mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasara yake.”—Mhubiri 8:9.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki