Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Nimeyatia Maneno Yangu Katika Kinywa Chako”
    Mungu Asema Nasi Kupitia Yeremia
    • Picha katika ukurasa wa 6

      6, 7. Tunajua jinsi gani kwamba Mungu alipendezwa na Yeremia, naye alizaliwa katika mazingira gani?

      6 Mume na mke wanapotazamia kupata mtoto, mara nyingi wao hufikiria sana maisha ambayo mwana au binti yao atakuwa nayo. Atakuwa mtu wa aina gani? Atakuwa na mapendezi, kazi na mafanikio gani? Haikosi wazazi wako waliyafikiria mambo hayo pia. Bila shaka wazazi wa Yeremia walimhangaikia pia. Hata hivyo, kisa chake ni cha pekee. Kwa nini? Muumba wa ulimwengu alipendezwa hasa na maisha na utendaji wa Yeremia.—Soma Yeremia 1:5.

      7 Hata kabla ya Yeremia kuzaliwa, Mungu alijua jinsi ambavyo maisha yake yangekuwa. Alipendezwa kwa njia ya pekee na mvulana huyo ambaye angezaliwa katika familia ya kikuhani iliyokuwa ikiishi upande wa kaskazini wa Yerusalemu. Wakati huo, katikati ya karne ya saba K.W.K., kulikuwa na taabu katika taifa la Yuda kwa sababu ya utawala mbaya wa Mfalme Manase. (Ona ukurasa wa 19.) Katika kipindi cha utawala wake wa miaka 55, Manase alifanya yaliyo mabaya machoni pa Yehova. Baadaye, mwana wake, Amoni, akawa vivyo hivyo. (2 Fal. 21:1-9, 19-26) Hata hivyo, wakati wa utawala wa mfalme wa Yuda aliyefuata kulikuwa na mabadiliko makubwa. Mfalme Yosia alimtafuta Yehova. Kufikia mwaka wa 18 wa utawala wake, Yosia alikuwa ameondolea mbali ibada ya sanamu. Lazima hilo liliwafurahisha wazazi wa Yeremia. Mungu alimpa utume mwana wao wakati wa utawala wa Yosia.—2 Nya. 34:3-8.

  • “Nimeyatia Maneno Yangu Katika Kinywa Chako”
    Mungu Asema Nasi Kupitia Yeremia
    • MUNGU ACHAGUA MSEMAJI

      8. Yeremia alipewa utume gani, naye aliitikiaje?

      8 Hatujui Yeremia alikuwa na umri gani Mungu alipomwambia: “Nilikufanya uwe nabii kwa mataifa.” Huenda alikuwa na umri wa miaka 25 hivi, umri ambao kuhani angeweza kuanza kutumikia. (Hes. 8:24) Vyovyote vile, Yeremia alisema: “Ole wangu, Ee Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova! Tazama, mimi hakika sijui jinsi ya kusema, kwa sababu mimi ni mvulana tu.” (Yer. 1:6) Alisita, labda akijiona kuwa mdogo mno au kwamba hastahili kutekeleza utume huo mzito kutia ndani kuzungumza mbele ya watu, kama makuhani walivyopaswa kufanya.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki