-
Yehova Hutoa Amani na Kweli kwa WingiMnara wa Mlinzi—1996 | Januari 1
-
-
“Nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli.”—YEREMIA 33:6.
-
-
Yehova Hutoa Amani na Kweli kwa WingiMnara wa Mlinzi—1996 | Januari 1
-
-
3. Katika utimizo wa maneno ya Yehova kupitia Yeremia, ni matukio gani ya kihistoria yaliyofundisha Israeli somo la pili lililo muhimu kuhusu amani?
3 Hata hivyo, kabla ya kuanguka kwa Yerusalemu, Yehova alikuwa amefunua kwamba yeye, wala si Misri, angeleta amani halisi Israeli. Kupitia Yeremia aliahidi: “Nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli. Nami nitawarudisha wafungwa wa Yuda, na wafungwa wa Israeli, na kuwajenga kama kwanza.” (Yeremia 33:6, 7) Ahadi ya Yehova ilianza kutimizwa katika 539 K.W.K. Babiloni liliposhindwa, na Waisraeli waliokuwa uhamishoni kupewa uhuru. (2 Mambo ya Nyakati 36:22, 23) Kufikia sehemu ya mwisho ya 537 K.W.K., kikundi cha Waisraeli kiliadhimisha Msherehekeo wa Mabanda katika Israeli kwa mara ya kwanza kwa miaka 70! Baada ya msherehekeo huo, walianza kujenga upya hekalu la Yehova. Walihisije kuhusu hilo? Rekodi yasema: ‘Walipaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi BWANA, kwa sababu msingi wa nyumba ya BWANA ulikwisha kuwekwa.’—Ezra 3:11.
-