-
Yehova Hutoa Tumaini Katikati ya MajonziMnara wa Mlinzi—1988 | Septemba 1
-
-
Yehova ni mwadilifu katika kuadhibu watenda makosa. Jambo hilo linakubaliwa wazi wakati Yerusalemu wenyewe unaponena. Huo unauliza kama kuna majonzi yo yote yaliyo kama umivu ambalo Mungu ameusababishia. Yeye ali peleka moto ulioliacha hekalu ukiwa. Dhambi za jiji zilikuja kuwa nira, na damu ilichururika kama utomvu wa matunda huku Mungu akikanyaga-kanyaga “shinikizo-divai” lao. Sayuni ilitandaza mikono kwa majonzi na kusihi kwa kujitetea isipate mfariji, na Yehova alikuwa mwadilifu katika kuadhibu Yerusalemu wenye uasi. Yeye na ashughulike vikali hivyo hivyo kwa maadui wake wenye kuchachawa.—1:12-22, NW.
-
-
Yehova Hutoa Tumaini Katikati ya MajonziMnara wa Mlinzi—1988 | Septemba 1
-
-
◻ 1:15, NW—‘Yehova alikuwa amekanyaga-kanyaga shinikizo-divai lenyewe lililokuwa la binti bikira wa Yuda’kwa sababu Yehova alikuwa ameamua na kuruhusu lililotukia. “Binti bikira wa Yuda” alikuwa Yerusalemu, uliofikiriwa kuwa kama mwanamke asiyenajisiwa. Wakati Wababuloni walipoharibu jiji hilo kuu la Yuda katika 607 K.W K., kulikuwa na umwagaji mkubwa wa damu, unaolinganika na kukamua umaji-maji wa matunda-zabibu katika shinikizo-divai. Yehova atahakikisha kwamba Jumuiya ya Wakristo, Yerusalemu ulio kifananishwa, utapondwa-pondwa vivyo hivyo
-