Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Nitamweka Mchungaji Mmoja”
    Hatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
    • Tai akiwa amebeba chipukizi la mwerezi kwenye makucha yake akielekea Babiloni.

      Tai mkubwa wa kwanza aliwakilisha Mfalme Nebukadneza wa Babiloni (Tazama fungu la 6)

      6. Fafanua maana ya fumbo hilo.

      6 Fumbo hilo lilimaanisha nini? (Soma Ezekieli 17:11-15.) Mwaka wa 617 K.W.K., Mfalme Nebukadneza wa Babiloni (“tai mkubwa” wa kwanza) alizingira Yerusalemu. Alimchukua Mfalme Yehoyakini wa Yuda (“chipukizi lililo juu zaidi”) kutoka kwenye kiti chake cha Ufalme na kumpeleka Babiloni (“jiji la wafanyabiashara”). Nebukadneza alimweka Sedekia (mmoja wa “mbegu za nchi” wa familia ya kifalme) awe mtawala huko Yerusalemu. Mfalme mpya wa Yuda aliapishwa katika jina la Mungu, na hivyo kuwajibika kuwa mshikamanifu akiwa mfalme kibaraka. (2 Nya. 36:13) Lakini Sedekia alipuuza kiapo chake; akaasi dhidi ya Babiloni na kugeukia Farao wa Misri (yule “tai mkubwa” wa pili) ili kupata msaada wa kijeshi lakini hakufanikiwa. Yehova alishutumu matendo yasiyo ya uaminifu ya Sedekia aliyevunja kiapo. (Eze. 17:16-21) Mwishowe, Sedekia aling’olewa mamlakani, na kufa gerezani huko Babiloni.—Yer. 52:6-11.

  • Unabii Kumhusu Masihi​—Mwerezi Mkubwa
    Hatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
      • Mkusanyo wa picha: 1. Tai akipanda mbegu katika shamba. 2. Mche wa mzabibu.

        2. Nebukadneza amweka Sedekia kuwa mtawala huko Yerusalemu

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki