Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Anachukia Ukosefu wa Haki
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 1
    • “MWANADAMU amemtawala mwanadamu kwa kumuumiza.” (Mhubiri 8:9) Maneno hayo yaliyoandikwa miaka 3,000 hivi iliyopita, yanaonyesha kwa usahihi hali katika ulimwengu tunaoishi. Wanadamu wana mwelekeo wa kutumia mamlaka vibaya bila kujali wao ni nani au wanaishi wapi. Mara nyingi wanawatendea isivyo haki watu wasio na uwezo na wanyonge. Yehova anahisije anapoona ukosefu huo wa haki? Tunapata jibu katika andiko la Ezekieli 22:6, 7, 31.​—Soma.

  • Yehova Anachukia Ukosefu wa Haki
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Agosti 1
    • Baada ya kusema hayo, Ezekieli anawashtaki viongozi na pia wale waliowaunga mkono kutotii Sheria za Yehova. Ezekieli anasema hivi: “Wamemtendea dharau baba na mama.” (Mstari wa 7) Kwa kudharau jukumu la wazazi, watu hao walivunja msingi wa taifa lao, yaani, familia.​—Kutoka 20:12.

      Watu hao wafisadi waliwadhulumu watu wanyonge waliokuwa miongoni mwao. Kila tendo la ukosefu wa sheria lilionyesha kwamba walidharau Sheria za Mungu kwa Waisraeli ambazo zilichochewa na upendo. Kwa mfano, Sheria ya Mungu iliwaagiza Waisraeli wawajali watu walioishi miongoni mwao ambao hawakuwa Waisraeli. (Kutoka 22:21; 23:9; Mambo ya Walawi 19:33, 34) Lakini watu hao walimtendea “kwa upunjaji” mkaaji mgeni.​—Mstari wa 7.

      Pia, watu hao waliwatendea vibaya watu ambao hawakuwa na mtu wa kuwalinda, yaani, “mvulana asiye na baba na mjane.” (Mstari wa 7) Yehova huwajali sana wale wanaofiwa na mzazi au mwenzi wa ndoa. Mungu aliahidi kwamba angewaadhibu watu ambao wangewatesa watoto au wajane wasio na mtu wa kuwalinda.​—Kutoka 22:22-24.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki