Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Nitawapa Moyo Wenye Umoja”
    Hatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
    • 36, 37. Ni ahadi gani zitakazotimizwa katika Paradiso wakati ujao?

      36 Baada ya vita vya Har–Magedoni, Yesu atafanya kihalisi kazi yake ya kurudisha katika dunia nzima. Wakati wa Utawala Wake wa Miaka Elfu Moja, atawaongoza wanadamu kuibadili dunia kuwa kama bustani ya Edeni, paradiso, kama vile ambavyo sikuzote Yehova amekusudia iwe! (Luka 23:43) Kisha wanadamu wote watakuwa na umoja kati yao wenyewe na pia dunia itakuwa makao salama. Hakutakuwa na hatari, wala vitisho mahali popote. Wazia wakati ambapo ahadi hii itatimizwa: “Nitafanya agano la amani pamoja nao, na kuwaondoa kabisa nchini wanyama hatari wa mwituni, ili wakae kwa usalama nyikani na kulala misituni.”—Eze. 34:25.

      37 Je, unaweza kuwazia hali hiyo? Utatembelea sehemu yoyote ya dunia hii kubwa bila kuogopa. Hakuna mnyama atakayekushambulia. Hakuna hatari itakayotishia amani yako. Utatembea peke yako katika msitu mkubwa, ukifurahia umaridadi wake, hata utalala huko ukiwa salama kabisa, ukiwa na hakika kwamba utaamka ukiwa umepumzika vya kutosha bila kushambuliwa!

      Msichana akiwa amelala chini ya mti usiku msituni. Chui mweusi akiwa amepumzika juu ya mti.

      Wazia wakati ambapo itakuwa salama “kulala misituni” (Tazama fungu la 36, 37)

  • “Nitawapa Moyo Wenye Umoja”
    Hatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki