Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2016 | Machi
    • Kwanza, tunasoma kwamba mifupa hiyo ilikuwa ama “imekauka” au “mikavu sana.” (Eze. 37:2, 11) Hilo linaonyesha kwamba mifupa hiyo ilikuwa ya watu ambao walikuwa wamekufa kwa muda mrefu sana. Pili, mifupa hiyo ilirudishiwa uhai hatua kwa hatua, si ghafla. Mwanzoni, kulikuwa na kelele, sauti ya kugongana, nayo “ikaanza kukaribiana, mfupa kwa mfupa.” Kisha, “kano na nyama” zikaongezwa. Halafu, mifupa, kano, na nyama zikafunikwa na ngozi. Mwishowe, “pumzi ikaanza kuingia ndani yao, nao wakaanza kuishi.” Kisha, Yehova akawaweka watu hao waliorudishiwa uhai katika nchi yao. Mambo hayo yote yangechukua wakati.—Eze. 37:7-10, 14.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2016 | Machi
    • Namna gani jambo la pili, yaani kurudishwa kwa watu wa Mungu? Jambo hilo lilitukia lini na jinsi gani? Kurudishwa kiroho kwa watu wa Mungu kulitokea hatua kwa hatua. Kuliambatana na “sauti ya kugongana” iliyotokea karne kadhaa kabla ya siku za mwisho kuanza. Ingawa mafundisho ya dini za uwongo yalikuwa na nguvu kwa muda mrefu, watu fulani waaminifu waliitetea ibada ya kweli kwa kadiri walivyoweza. Baadhi yao walijitahidi kutafsiri na kuchapisha Biblia katika lugha ambayo watu wengi walielewa. Wengine walitangaza kweli ambazo walikuwa wamegundua katika Neno la Mungu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki