-
“Nitawafanya Kuwa Taifa Moja”Hatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
-
-
4. Jambo ambalo Ezekieli anafanya akitumia vijiti viwili linamaanisha nini? (Tazama picha mwanzoni mwa sura hii.)
4 Ezekieli aliagizwa aviunganishe vijiti hivyo pamoja “ili viwe kijiti kimoja tu.” Wahamishwa walipokuwa wakimtazama Ezekieli, walimuuliza: “Je, hutatuambia mambo haya yanamaanisha nini?” Alijibu kwamba mambo aliyoigiza yalionyesha jambo ambalo Yehova angefanya. Yehova alisema hivi kuhusu vile vijiti viwili: “Nitavifanya viwe kijiti kimoja, navyo vitakuwa kijiti kimoja mkononi mwangu.”—Eze. 37:17-19.
5. Ni nini maana ya jambo ambalo Ezekieli aliigiza? (Tazama sanduku “Kuunganishwa kwa Vijiti Viwili.”)
5 Kisha, Yehova akafafanua maana ya kuunganishwa kwa vijiti viwili. (Soma Ezekieli 37:21, 22.) Wahamishwa kutoka ufalme wenye makabila mawili wa Yuda na wahamishwa kutoka ufalme wenye makabila kumi wa Israeli (Efraimu) wangerudi katika nchi ya Israeli, ambako wangekuwa “taifa moja.”—Yer. 30:1-3; 31:2-9; 33:7.
-
-
Kuunganishwa kwa Vijiti ViwiliHatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
-
-
“viwe kijiti kimoja tu mkononi mwako”
NYAKATI ZA KALE
537 K.W.K. Waabudu wa kweli warudi kutoka katika mataifa, wajenga upya Yerusalemu, na kuabudu wakiwa taifa moja.
NYAKATI ZA KISASA
Tangu 1919, watu wa Mungu wanapangwa hatua kwa hatua na kuunganishwa ili watumikie wakiwa “kundi moja.”
-