-
Lile “Hekalu” na Yule “Mkuu” LeoMnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
-
-
3. Twajifunza nini kutokana na dari refu na michoro iliyo ukutani katika vijia vya kuingia hekaluni?
3 Wazia kwamba tunazuru hekalu hilo la kimaono. Twakaribia na kupanda vipandio saba hadi kwenye moja la hayo malango makubwa mno. Tukiwa ndani ya kijia hicho cha kuingilia, twatazama juu kwa kuduwaa. Dari lake lina urefu wa meta 30 kwenda juu! Hivyo, twakumbushwa kwamba viwango vya kuingia katika mpango wa Yehova wa ibada ni vya juu sana. Miali ya nuru inayopenyeza kutoka madirishani yamulika michoro ya mitende iliyo ukutani, ambayo hutumiwa katika Maandiko kufananisha unyofu. (Zaburi 92:12; Ezekieli 40:14, 16, 22) Mahali hapo patakatifu ni pa wale walio wanyofu kiadili na kiroho. Kwa kupatana na hilo, twataka kubaki tukiwa wanyofu ili ibada yetu ikubalike kwa Yehova.—Zaburi 11:7.
-
-
Lile “Hekalu” na Yule “Mkuu” LeoMnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
-
-
5. (a) Ni ufanano gani uliopo kati ya ono la Ezekieli na ono la Yohana ambalo limerekodiwa kwenye Ufunuo 7:9-15? (b) Katika ono la Ezekieli, makabila 12 yanayoabudia kwenye ua wa nje yafananisha nani?
5 Kijia hicho chaelekeza kwenye ua wa nje ambapo watu wamwabudu na kumsifu Yehova. Hilo latukumbusha juu ya ono la mtume Yohana la “umati mkubwa” ukimwabudu Yehova “mchana na usiku katika hekalu lake.” Mitende yaonyeshwa katika maono yote mawili. Katika ono la Ezekieli hiyo yapamba kuta za kijia cha kuingilia. Katika ono la Yohana waabudu wana matawi ya mitende mikononi mwao, ikionyesha shangwe yao katika kumsifu Yehova na kumkaribisha Yesu akiwa Mfalme wao. (Ufunuo 7:9-15) Katika muktadha wa ono la Ezekieli, yale makabila 12 ya Israeli yafananisha “kondoo wengine.” (Yohana 10:16; linganisha Luka 22:28-30.) Je, wewe ni mmoja wa wale wanaopata shangwe katika kumsifu Yehova kwa kutangaza Ufalme wake?
-