Maandishi ya kale ya Babiloni yanataja mara kadhaa visa vya kuwaua watu kwa kuwatupa kwenye tanuru lenye moto, kutia ndani visa ambavyo maagizo kama hayo yalitolewa na watawala. Hati moja ya zamani inayoaminiwa kuwa ya kipindi cha Nebukadneza, inaeleza kuhusu adhabu waliyopewa maofisa walioshtakiwa kwamba wamekufuru miungu ya Babiloni. Hati hiyo inasema: “Waangamize, wachome, waunguze. . . katika jiko la mpishi . . . moshi mwingi na upae, wateketeze kwa moto mkali.”