-
Maneno Manne Yaliyoubadili UlimwenguSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
6 Hata hivyo, Belshaza bado alikuwa akifikiria tendo jingine lililokuwa lenye ufidhuli hata zaidi. “Mfalme na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake . . . wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe.” (Danieli 5:3, 4) Kwa hiyo, Belshaza alinuia kukweza miungu yake isiyo ya kweli juu kuliko Yehova! Yaonekana Wababiloni wengi walikuwa na mtazamo huo. Waliwadharau mateka wao Wayahudi, wakidhihaki ibada yao na kutowapa matumaini yoyote ya kurudi nyumbani kwao walikokupenda. (Zaburi 137:1-3; Isaya 14:16, 17) Huenda mtawala huyo aliyelewa chakari alihisi kwamba kuwadhili wahamishwa hao na kumtukana Mungu wao kungewavutia wanawake wake na mawaziri wake, na kufanya aonekane kuwa mwenye nguvu.a Lakini hata ikiwa Belshaza alisisimuka kwa kuhisi kwamba alikuwa na nguvu, hilo halikudumu.
-
-
Maneno Manne Yaliyoubadili UlimwenguSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
a Katika maandishi ya kale, Mfalme Koreshi alisema hivi juu ya Belshaza: “Mtu mnyonge amewekwa kuwa [mtawala] wa nchi yake.”
-