-
Kitabu cha Danieli ChashtakiwaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
7. (a) Kwa nini wachambuzi wa Biblia wamependezwa kwa muda mrefu na jinsi Danieli anavyomtaja Belshaza mara kadhaa? (b) Dhana ya kwamba Belshaza alikuwa mtu bandia ilipatwa na nini?
7 Danieli aliandika kwamba Belshaza, “mwana” wa Nebukadreza, alikuwa akitawala Babiloni akiwa mfalme wakati jiji hilo lilipopinduliwa. (Danieli 5:1, 11, 18, 22, 30) Kwa muda mrefu, wachambuzi wameishambulia taarifa hiyo, kwa kuwa jina la Belshaza halikupatikana kwingineko isipokuwa katika Biblia. Badala yake, wanahistoria wa kale walimtambulisha Nabonido, mwandamizi wa Nebukadreza, kuwa mfalme wa mwisho wa Babiloni. Kwa hiyo, mwaka wa 1850, Ferdinand Hitzig alisema kwamba kwa wazi Belshaza alibuniwa na mwandikaji. Lakini, je, maoni ya Hitzig hayaonekani kuwa ya haraka-haraka tu? Je, kwani kukosa kutajwa popote kwa mfalme huyo—hasa wakati ambapo yakubalika kwamba rekodi za historia zilikuwa chache—kwa kweli kungethibitisha kwamba hakupata kuishi kamwe? Haidhuru, mwaka wa 1854 silinda kadhaa ndogo za udongo zilifukuliwa kwenye magofu ya Uru, jiji la Babiloni la kale, mahali ambapo sasa ni sehemu ya kusini ya Iraki. Hati hizo za kikabari za Mfalme Nabonido zilitia ndani sala kwa niaba ya “Bel-sar-ussur, mwanangu mkubwa.” Hata wachambuzi walilazimika kukubali: Huyo ndiye aliyekuwa Belshaza wa kitabu cha Danieli.
-
-
Kitabu cha Danieli ChashtakiwaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
9. (a) Ni katika maana gani ambayo huenda Danieli alimaanisha kwamba Belshaza alikuwa mwana wa Nebukadreza? (b) Kwa nini wachambuzi hukosea kusisitiza kwamba Danieli hata hadokezi kuwepo kwa Nabonido?
9 Wakiwa hawajaridhika bado, wachambuzi fulani hudai kwamba Biblia haimwiti Belshaza mwana wa Nabonido, bali mwana wa Nebukadreza. Wengine husisitiza kwamba kitabu cha Danieli hata hakitaji kuweko kwa Nabonido. Hata hivyo, vipingamizi vyote viwili havithibitiki vichunguzwapo. Yaonekana Nabonido alimwoa binti ya Nebukadreza. Hilo lingemaanisha kwamba Belshaza ni mjukuu wa Nebukadreza. Lugha ya Kiebrania wala ya Kiaramu hazina neno “babu” au “mjukuu”; mtajo “mwana wa” ungeweza kumaanisha “mjukuu wa” au hata “mzao wa.” (Linganisha Mathayo 1:1.) Isitoshe, masimulizi ya Biblia hukubali Belshaza atambulishwe kuwa mwana wa Nabonido. Alipoogofywa na mwandiko ukutani wenye kuashiria mabaya, Belshaza asiye na tumaini amwahidi yeyote awezaye kufasiri maana ya maneno hayo, cheo cha tatu katika ufalme. (Danieli 5:7) Mbona cheo cha tatu wala si cha pili? Ahadi hiyo yadokeza kwamba cheo cha kwanza na cha pili vilikuwa vimechukuliwa tayari. Kwa kweli, vilikuwa vimechukuliwa na Nabonido na mwana wake, Belshaza.
-