-
Wakati Yehova Wafalme Masomo AlipofunzaMnara wa Mlinzi—1988 | Desemba 1
-
-
15. Belshaza alionyeshaje madharau kwa Mungu wa kweli, Yehova?
15 Mfalme mwingine ambaye Yehova alipata pindi ya kumfunza alikuwa Belshaza. Yeye alikuwa mwana na mtawala-mwenzi wa Mfalme Nabonido, huyo naye akiwa ni mwana wa Nebukadreza. Katika pindi ya karamu kubwa, Belshaza alithubutu kufanya kiherehere cha kuagiza vyombo vya dhahabu ambavyo babu yake alikuwa ametoa katika hekalu la Yehova katika Yerusalemu viletwe ndani ili yeye, waheshimiwa wake, wake zake, na masuria wake wavinywee. Kwa hiyo “wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe.”—Danieli 5:3, 4.
-
-
Wakati Yehova Wafalme Masomo AlipofunzaMnara wa Mlinzi—1988 | Desemba 1
-
-
17 Danieli alizidi kumwambia Belshaza hivi: “Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.” (Danieli 5:23) Kwa hiyo mwandiko huo ulimpa ilani mtawala huyo wa Babuloni kwamba siku za umaliki wake zilikuwa zimefika ukingoni, kwamba yeye alikuwa amepimwa katika mizani na kupatikana mpungukiwa, na kwamba ufalme wake ungepewa kwa Wamedi na Waajemi. Na usiku huo huo, baada ya Yehova kuwa amefunza mfalme huyo mwenye kiburi somo hilo lililohitajika sana, Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, aliuawa.—Danieli 4:23.
-