Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Aokolewa Asiliwe na Simba!
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 20. Ni nini kilichowapata adui za Danieli waliokuwa na uchungu na uovu?

      20 Sasa, kwa kuwa Danieli alikuwa salama salimini, Dario akawa na shughuli nyingine. “Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.”d—Danieli 6:24.

      21. Katika kushughulika na washiriki wa familia za wakosaji, ni tofauti gani iliyokuwapo kati ya Sheria ya Kimusa na sheria za tamaduni fulani za kale?

      21 Huenda kuua wapanga-njama pamoja na wake zao na watoto wao kukaonwa kuwa ukali wa kupita kiasi. Kinyume cha hilo, Sheria ambayo Mungu alitoa kupitia nabii Musa ilitaarifu hivi: “Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu na auawe kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.” (Kumbukumbu la Torati 24:16) Hata hivyo, katika tamaduni fulani za kale, kwa kawaida washiriki wa familia waliuawa pamoja na mkosaji, ikiwa alifanya kosa kubwa. Huenda hilo lilifanywa ili washiriki wa familia wasiweze kulipiza kisasi baadaye. Hata hivyo, tendo hilo dhidi ya familia za mawaziri na maliwali halikusababishwa na Danieli. Yaelekea, Danieli alisononeshwa na maafa ambayo watu hao waovu walikuwa wamesababishia familia zao.

  • Aokolewa Asiliwe na Simba!
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • d Neno “waliomshitaki” latafsiriwa kutokana na usemi wa Kiaramu ambao pia waweza kutafsiriwa “waliomchongea.” Hilo laonyesha nia mbovu ya adui za Danieli.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki