Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Unabii Mwingi Uliotimizwa
    Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu?
    • 22. Katika unabii wenye kuhusiana wa mwendo wa mamlaka za ulimwengu, ni mamlaka ya ulimwengu nyingine gani iliyotolewa unabii?

      22 Katika Danieli sura 7, njozi inayokaribia kufanana na hiyo ilitazama pia wakati ujao ulio mbali. Mamlaka ya ulimwengu ya Kibabuloni ilifananishwa na simba, ile ya Uajemi na dubu, na ile ya Ugiriki na chui mwenye mabawa manne mgongoni mwake na vichwa vinne. Kisha, Danieli aona hayawani-mwitu mwingine, “mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi . . . , naye alikuwa na pembe nne.” (Danieli 7:2-7) Hayawani-mwitu huyo wa nne alifananisha Milki ya Kiroma yenye nguvu nyingi, iliyoanza kusitawi karibu karne tatu baada ya Danieli kuandika unabii huo.

  • Unabii Mwingi Uliotimizwa
    Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu?
    • 24, 25. (a) Zile pembe kumi za hayawani-mwitu zilijitokezaje? (b) Danieli alitangulia kuona mng’ang’ano gani kati ya pembe za hayawani-mwitu?

      24 Ingawa hivyo, vipi juu ya pembe kumi za hayawani huyu mkubwa? Malaika alisema: “Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” (Danieli 7:24) Hayo yalitimiaje?

      25 Basi, wakati Milki ya Kirumi ilipoanza kuzorota katika karne ya tano W.K., mahali payo hapakuchukuliwa mara moja na mamlaka nyingine ya ulimwengu. Badala yake, ilivunjika-vunjika kuwa falme kadha wa kadha, “wafalme kumi.” Mwishowe, Milki ya Uingereza ilishinda zile milki tatu zenye kushindana nayo za Hispania, Ufaransa, Uholanzi ikawa mamlaka kuu ya ulimwengu. Hivyo ndivyo “pembe” hii mpya ilivyoshusha hao “wafalme watatu.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki