Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ni Nani Awezaye Kusimama Dhidi ya mkuu wa Wakuu?
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 21. Ni nani wanaomiliki “patakatifu” ambapo serikali ya ulimwengu ya saba hujaribu kufanya ukiwa?

      21 Leo mabaki ya 144,000 ni wawakilishi wa kidunia wa “Yerusalemu la kimbingu”—Ufalme wa Mungu ulio kama jiji—na mpango wake wa hekalu. (Waebrania 12:22, 28; 13:14) Vivyo hivyo, wapo “patakatifu” ambapo serikali ya ulimwengu ya saba hujaribu kukanyaga-kanyaga na kupafanya ukiwa. (Danieli 8:13) Akinena juu ya mahali hapo patakatifu kwamba ni “mahali pa patakatifu pake [Yehova],” Danieli asema hivi: “Ikamwondolea [Yehova] sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini. Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa.” (Danieli 8:11, 12) Hilo lilitimizwaje?

      22. Wakati wa Vita ya Ulimwengu ya Pili, ile serikali ya ulimwengu ya saba ilifanya “makosa” gani yenye kuonekana wazi?

      22 Mashahidi wa Yehova walipatwa na nini wakati wa Vita ya Ulimwengu ya Pili? Walinyanyaswa vikali! Mnyanyaso ulianzia nchi za Nazi na za Ufashisti. Lakini punde si punde ‘kweli iliangushwa hata chini’ kotekote katika milki hiyo kubwa ya ‘pembe ndogo iliyokuwa imepata nguvu nyingi.’ “Jeshi” la wapiga-mbiu wa Ufalme na kazi yao ya kuhubiri “habari njema” lilipigwa marufuku katika karibu nchi zote za Jumuiya ya Madola ya Uingereza. (Marko 13:10) Mataifa hayo yalipopanga mbinu zao za kivita, yalikataa kuwapa Mashahidi wa Yehova uhuru wa wahudumu wa kutoshiriki utumishi wa kijeshi, wakionyesha kutostahi hata kidogo kuwekwa kwao kitheokrasi kuwa wahudumu wa Mungu. Watumishi waaminifu wa Yehova huko Marekani walitendewa jeuri na vikundi vya wafanya-ghasia na kuvunjiwa adhama kwa njia mbalimbali. Serikali ya ulimwengu ya saba, kwa hakika, ilijaribu kuondoa dhabihu ya sifa—“tunda la midomo”—ambayo watu wa Yehova walimtolea kwa ukawaida ikiwa “ya daima” katika ibada yao. (Waebrania 13:15) Kwa hiyo, serikali hiyo ya ulimwengu ilifanya “makosa” ya kuvamia milki halali ya Mungu Aliye Juu—“mahali pa patakatifu pake.”

      23. (a) Wakati wa Vita ya Ulimwengu ya Pili, Serikali ya Ulimwengu ya Uingereza na Marekani ‘ilishindanaje na Mkuu wa wakuu’? (b) “Mkuu wa wakuu” ni nani?

      23 Kwa kuwanyanyasa “watakatifu” wakati wa Vita ya Ulimwengu ya Pili, ile pembe ndogo ilijitukuza “hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo.” Au, kama vile malaika Gabrieli anavyotaarifu, ilisimama “kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu.” (Danieli 8:11, 25) Jina la cheo “Mkuu wa wakuu” hutumika kwa Yehova Mungu peke yake. Neno la Kiebrania sar, linalotafsiriwa “mkuu,” lahusiana na neno linalomaanisha “tawala.” Zaidi ya kurejezea mwana wa mfalme au mtu mwenye wadhifa wa kifalme, neno hilo hutumika kurejezea kiongozi, au jumbe. Kitabu cha Danieli huwataja malaika wengine walio wakuu—kwa kielelezo, Mikaeli. Mungu ndiye Mkuu Zaidi wa wakuu hao. (Danieli 10:13, 21; linganisha Zaburi 83:18.) Je, twaweza kumwazia mtu awaye yote akishindana na Yehova—Mkuu wa wakuu?

      “PATAKATIFU” PATAKASWA

      24. Danieli 8:14 hutuhakikishia nini?

      24 Hakuna awezaye kushindana na Mkuu wa wakuu—hata mfalme mwenye “uso mkali” kama vile Serikali ya Ulimwengu ya Uingereza na Marekani! Mfalme huyo hapati mafanikio katika kujaribu kwake kufanya ukiwa patakatifu pa Mungu. Baada ya kipindi cha “jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu,” asema malaika mjumbe, ‘patakatifu patatakaswa,’ au “patashinda.”—Danieli 8:13, 14; The New English Bible.

  • Ni Nani Awezaye Kusimama Dhidi ya mkuu wa Wakuu?
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 27. Kulikuwa na uthibitisho gani wa kwamba “sadaka ya kuteketezwa daima” ilizuiliwa katika miaka iliyojaa minyanyaso wakati wa Vita ya Ulimwengu ya Pili?

      27 Ingawa zile siku 2,300 zilimalizika wakati wa Vita ya Ulimwengu ya Pili, iliyoanza mwaka wa 1939, kutolewa kwa “sadaka ya kuteketezwa ya daima” kwenye patakatifu pa Mungu kulizuiwa sana kwa sababu ya mnyanyaso. Mwaka wa 1938, Watch Tower Society ilikuwa na ofisi za tawi 39 zilizokuwa zikisimamia kazi ya Mashahidi ulimwenguni pote, lakini kufikia mwaka wa 1943 zilikuwa 21 tu. Pia, idadi ya wapiga-mbiu wa Ufalme wakati huo haikuongezeka sana.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki