Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ugiriki—Ile Serikali Kubwa ya Tano ya Ulimwengu
    Mnara wa Mlinzi—1988 | Aprili 15
    • Katika njozi ya pili ya kiunabii, mbuzi wa kiume (beberu) alionwa ‘akija kutoka machweo ya jua [magharibi] juu ya uso wa dunia nzima,” akienenda kwa mwendo wa kasi sana hivi kwamba “hakuwa akigusa dunia.” Alikuja njia yote ile mpaka kwa yule kondoo wa kiume ambaye malaika alisema “anasimamia wafalme wa Umedi na Uajemi.” Huyo mbuzi wa kiume “akaendelea na kupigisha chini yule kondoo wa kiume na kuvunja pembe mbili zake.” Danieli aliambiwa: “Yule mbuzi-mume mwenye nywele-nywele anasimamia mfalme wa Ugiriki.”—Danieli 8:5-8, 20, 21, NW.

  • Ugiriki—Ile Serikali Kubwa ya Tano ya Ulimwengu
    Mnara wa Mlinzi—1988 | Aprili 15
    • Maunabii Yatimizwa

      Katika masika ya mwaka 334 K.W.K., Aleksanda aliingia Esia kule Dardanelles (ile Hellespont ya kale) akiwa na askari 30,000 watembea-miguu na wapanda-farasi 5,000. Akiwa na mwendo wa chui mfananishwa, mwenye mabawa manne, au mwendo wa mbuzi ambaye alionekana kama kwamba hagusi chini, yeye alikumba maeneo yote ya milki ya Uajemi—iliyokuwa na ukubwa ulio mara 50 za ufalme wake mwenyewe! Je! yeye ‘angetawala akiwa na eneo lililoenea sana na kufanya kulingana na mapenzi yake’? Historia inajibu.

      Kwenye Mto Graniko katika pembe ya kaskazini-magharibi ya Esia Ndogo (Uturuki ya ki-siku-hizi) Aleksanda alishinda pigano lake la kwanza dhidi ya Waajemi. Wakati wa kipupwe hicho, yeye alishinda Esia Ndogo ya magharibi. Vuli iliyofuata, kule Issus katika pembe ya kusini-mashariki ya Esia Ndogo, yeye alishinda kabisa kabisa jeshi la Kiajemi lililokadiriwa kuwa wanaume nusu-milioni, na yule mfalme mkuu, Dario 3 wa Uajemi, akakimbia, akiacha jamaa yake kwenye mikono ya Aleksanda.

      Badala ya kufuatia Waajemi wenye kukimbia, Aleksanda alipiga miguu kuelekea kusini kando-kando ya pwani ya Mediterania, akishinda vituo vikuu vilivyotumiwa na kile kikosi chenye nguvu cha meli za Kiajemi. Mji Tiro wa kisiwani ulikinza kwa miezi saba. Mwishowe kabisa, akitumia mabomoko ya ule mji-bara wa zamani ambao Nebukadreza alikuwa ameharibu, Aleksanda akajenga pito la kwenda nje kwenye mji wa kisiwani. Mabakio ya pito hilo yanaonekana leo, yakishuhudiza utimizo wa unabii wa Ezekieli kwamba mavumbi ya Tiro yangesukumizwa ndani ya bahari.​—Ezekieli 26:4, 12.

  • Ugiriki—Ile Serikali Kubwa ya Tano ya Ulimwengu
    Mnara wa Mlinzi—1988 | Aprili 15
    • Shabaha zote za mpangilio wa Philip zilikuwa zimetimizwa kwa kuzidi, lakini Aleksanda alikuwa bado hajamaliza mambo. Akiwa kama mbuzi-mume mwenye kuenenda kasi, yeye aligeuka kuelekea nyuma kaskazini-mashariki, kupitia Palestina na kupanda juu kuelekea Mto Tigri. Huko, katika mwaka 331 K.W.K., yeye alihusisha Waajemi vitani kule Gaugamela, si mbali na yale magofu yenye kumumunyika ya uliokuwa mji mkuu wa Kiashuri, Ninawi. Wanaume 47,000 wa Aleksanda walilemea jeshi la Kiajemi lililopangwa upya, la watu 1,000,000. Dario 3 alikimbia na baadaye akauawa na watu wake mwenyewe.

      Akiwa anabubujika ushindi, Aleksanda aligeukia kusini na kutwaa Babuloni, mji mkuu wa Kiajemi wakati wa kipupwe. Pia alichukua ukazi wa miji mikuu huko Susa na Persepolisi, akibamba ile hazina kubwa sana ya Kiajemi na kuchoma jumba kuu la mfalme Zakse. Mwishowe kabisa, mji mkuu huko Ekbatana ulianguka mikononi mwake. Ndipo mshindaji huyo mwenye mwendo wa kasi alipoiweka chini yake sehemu iliyobaki ya eneo la utawala wa Kiajemi, lenye kufika mbali mpaka mashariki ya Mto Indus katika Pakistan ya ki-siku-hizi. Pasipo swali, Ugiriki ilikuwa imekuja kuwa ya tano ya zile serikali kubwa za ulimwengu katika historia ya Biblia.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki