Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ni Nani Ataongoza Mataifa Kwenye Amani?
    Je! Ulimwengu Usio na Vita Utakuwako Wakati Wowote?
    • Majuma sabini: Waelezaji wa Kiyahudi karibu wote huelewa hayo yakimaanisha majuma ya miaka, yaani, miaka 490. Hilo lapatana na hesabu ya kiunabii ya Kimaandiko kwa “mwaka mmoja kwa kila siku moja.”—Hesabu 14:34; Mambo ya Walawi 25:8; Ezekieli 4:6.

      “Tangu kutolewa kwa lile neno la kurudisha na kujenga Yerusalemu” (Danieli 9:25, JP): Nehemia husimulia kwamba katika mwaka wa 20 wa Mfalme Artasaksi, alipewa utume wa kurudisha na kujenga upya Yerusalemu. Hiyo ilikuwa katika mwaka 455 K.W.K.—Nehemia 2:1-8; ona Insight on the Scriptures, Buku 2, kurasa 614-16, 899-900, kilichotangazwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

      Majuma saba: Majuma saba (ya miaka, au miaka 49) huhusiana na kipindi cha kukamilisha kurudishwa kwa jiji, Yerusalemu.

      Majuma sitini na mawili: Majuma sitini na mawili (ya miaka, au miaka 434) huhusiana na kile kipindi cha baada ya kukamilishwa kwa jiji mpaka kuja kwa yule Mesiya.i

      Kwa kujumlisha vipindi hivyo viwili vya wakati pamoja, mtu hufikia majuma 69 ya miaka, au miaka 483. Kuhesabu kutoka mahali pa kuanzia pa 455 K.W.K. huonyesha mwisho wa juma la 69 kuwa 29 W.K.

      29W.K.: Myahudi aitwaye Yesu (Kiebrania, Yeshua), aliyezaliwa katika Bethlehemu na kulelewa katika Nazareti, kutoka nasaba ya Daudi, aanza kuhubiri kotekote katika nchi ya Israeli.—Luka 3:1-3, 21, 22.

  • Ni Nani Ataongoza Mataifa Kwenye Amani?
    Je! Ulimwengu Usio na Vita Utakuwako Wakati Wowote?
    • i Zile alama za vituo zipatikanazo katika maandishi-awali ya Kiebrania cha kisasa (maandishi-awali ya Kiebrania cha awali hayakuwa na nukta za irabu au alama za vituo), ambazo husababisha uelewevu tofauti wa ugawanyaji huu wa wakati, si za awali bali ni nyongeza ya waandishi katika zile Enzi za Katikati ambao kwa wazi walifanya hivyo kwa kuwa fasiri ya andiko hilo ilionekana kuwa ilitimizwa katika Yesu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki