Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Watiwa Nguvu na Mjumbe Kutoka Kwa Mungu
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 9, 10. (a) Danieli alikuwa wapi alipoona ono? (b) Fafanua kile ambacho Danieli aliona kwenye ono.

      9 Danieli hatamaushwi. Anatuambia kifuatacho kutokea, akisema hivi: “Nilipokuwa kando ya ule mto mkubwa, Hidekeli; naliinua macho yangu, nikatazama, na kumbe, mtu aliyevikwa nguo za kitani, viuno vyake vimefungwa dhahabu safi ya Ufazi.” (Danieli 10:4, 5) Hidekeli ulikuwa mmojawapo wa mito minne iliyotoka kwenye bustani ya Edeni. (Mwanzo 2:10-14) Katika Kiajemi cha Kale, Hidekeli uliitwa Tigra, litokapo jina la Kigiriki, Tigris. Eneo lililo kati ya Hidekeli na Eufrati lilikuja kuitwa Mesopotamia, yaani “Nchi Iliyo Katikati ya Mito.” Hilo lathibitisha kwamba Danieli alipoona ono hilo, bado alikuwa Babilonia, ingawa huenda hakuwa katika jiji la Babiloni.

  • Watiwa Nguvu na Mjumbe Kutoka Kwa Mungu
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 12, 13. Ni nini kinachoonyeshwa na (a) mavazi ya mjumbe? (b) sura ya mjumbe?

      12 Acheni tumchunguze kwa makini mjumbe huyo mwenye kuvutia aliyemwogofya Danieli kiasi hicho. Alikuwa ‘amevikwa nguo za kitani, viuno vyake vikiwa vimefungwa dhahabu safi ya Ufazi.’ Katika Israeli la kale, mshipi, naivera, na kifuko cha kifuani za kuhani wa cheo cha juu, na pia majoho ya makuhani wengine, zilitengenezwa kwa kitani nzuri na kurembeshwa kwa dhahabu. (Kutoka 28:4-8; 39:27-29) Kwa hiyo, mavazi ya mjumbe huyo yaonyesha alikuwa na wadhifa mtakatifu na wa adhama.

      13 Danieli alitiwa kicho pia na sura ya mjumbe huyo—kung’aa kwake kana kwamba alikuwa na mwili wa vito, kumulika sana kwa uso wake mwangavu, uwezo wenye kupenya wa macho yake yaliyo kama taa za moto, na mng’ao wa mikono na miguu yake yenye nguvu. Hata sauti yake yenye kuamuru ilikuwa yenye kutia kicho. Yote hayo yaonyesha waziwazi kwamba alikuwa na uwezo upitao wa kibinadamu. ‘Mtu huyo aliyevikwa nguo za kitani’ hakuwa mwingine ila malaika mwenye wadhifa mkubwa, aliyetumikia katika kuwapo kutakatifu kwa Yehova, alipotoka na ujumbe.a

  • Watiwa Nguvu na Mjumbe Kutoka Kwa Mungu
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • a Ingawa malaika huyo hatajwi kwa jina, yaonekana ndiye yuleyule ambaye sauti yake ilisikiwa ikimwagiza Gabrieli amsaidie Danieli kuhusu lile ono ambalo alikuwa ametoka tu kuona. (Linganisha Danieli 8:2, 15, 16 na Danieli 12:7, 8.) Isitoshe, Danieli 10:13 huonyesha kwamba Mikaeli, “mmoja wa hao wakuu wa mbele,” alikuja kumsaidia malaika huyo. Kwa hiyo, malaika huyo asiyetajwa kwa jina lazima alikuwa na pendeleo la kufanya kazi bega kwa bega na Gabrieli na Mikaeli.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki