Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kung’ang’ania Mamlaka ya Duniani Pote Ni Nani Atakayeshinda?
    Mnara wa Mlinzi—1986 | Oktoba 15
    • Ikiwa wewe umesoma historia ya Ugiriki ya Kale, unajua kwamba Aleksanda Mkuu alilifanya taifa hilo likawa milki ya kifalme. Jambo hilo lilitabiriwa na Danieli nabii wa Biblia. Kulingana na ilivyokuwa imetabiriwa na unabii huo, baada ya huyo ‘mfalme hodari’ kufa mwaka 323 K.W.K., mwishowe milki hiyo ‘iligawanyika kuzielekea zile pepo nne’​—kati ya wanne wa majenerali wake. (Danieli 11:2-4) Kati ya hao, Seleuko Niketa wa Kwanza alianza kutawala Siria na Mesopotamia​—maeneo yaliyo kaskazini na mashariki mwa nchi ya nyumbani kwa Danieli, yaani, Yuda. Tolemi Lago, jenerali mwingine Mgiriki, alianza kutawala Misri na Palestina, na hivyo akawa kusini na magharibi mwa eneo la utawala wa Seleuko Niketa. Upande ambao kila mmoja wao alikuwa ndio uliowafanya wakawa “mfalme wa kaskazini” na “mfalme wa kusini.”​—Danieli 11:5, 6.

      “Kaskazini” na “kusini” zikaja kufananisha mataifa yenye nguvu nyingi yaliyojazia vyeo fulani vya kiunabii.a Katika muda wa karne zilizofuata, mataifa tofauti-tofauti yamejazia vyeo vya “wafalme” hao wawili; lakini sikuzote mataifa hayo yamefanana na maelezo ya kiunabii yanayoyahusu. Sikuzote yametambuliwa kwa sababu ya ushindani yalio nao, hali kwa kawaida yamekuwa yakitawala maeneo yaliyo kaskazini na kusini mwa taifa lile jingine.

      Leo vyeo hivyo vinalingana na yale majina “Mashariki” na “Magharibi.” Hiyo, pia, ni mitajo ya mfano, kwa sababu maeneo yanayohusika yamepitana-pitana. Mitajo hii ya Kibiblia “kaskazini” na “kusini” ni mifano inayofaa pia ijapokuwa hiyo vilevile imepitana-pitana.

  • Kung’ang’ania Mamlaka ya Duniani Pote Ni Nani Atakayeshinda?
    Mnara wa Mlinzi—1986 | Oktoba 15
    • a Kwa mfano, yale maneno yanayosema “ndipo badala yake atasimama mmoja” yanamaanisha kuchukua cheo cha “mfalme wa kaskazini.”​—Danieli 11:20, 21

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki