Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Bibi Mwenye Nywele Nyeusi wa Jangwa la Siria”
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Januari 15
    • Fursa ya Zenobia ya kupanua mamlaka yake ya kifalme ilikuja katika 269 W.K., wakati msingiziaji mmoja aliyekuwa akishindania utawala wa Roma alipotokea katika Misri. Jeshi la Zenobia liliingia Misri mara moja, likamaliza mwasi huyo, nalo likatwaa nchi hiyo. Akijitangaza mwenyewe kuwa malkia wa Misri, alipiga chapa sarafu kwa jina lake. Sasa ufalme wake ulienea kutoka mto Naili hadi mto Frati. Kufikia hatua hii maishani mwake, alikuja kuwa “mfalme wa kusini” anayesemwa katika unabii wa Biblia wa Danieli, kwa kuwa ufalme wake huo ulitawala eneo la kusini la nchi ya nyumbani ya Danieli. (Danieli 11:25, 26) Pia alishinda sehemu kubwa zaidi ya Asia Ndogo.

  • “Bibi Mwenye Nywele Nyeusi wa Jangwa la Siria”
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Januari 15
    • Maliki ‘Achochea Moyo Wake’ Dhidi ya Zenobia

      Katika 270 W.K., Aurelian akawa maliki wa Roma. Majeshi yake yalishinda kwa mafanikio na kutia nidhamu wakatili wa kaskazini. Katika 271 W.K.—sasa akiwakilisha “mfalme wa kaskazini” wa unabii wa Danieli—Aurelian ‘alichochea mamlaka yake na moyo wake dhidi ya mfalme wa kusini,’ aliyewakilishwa na Zenobia. (Danieli 11:25a) Aurelian alituma baadhi ya majeshi yake moja kwa moja hadi Misri na kuongoza jeshi lake kuu kuelekea mashariki kupitia Asia Ndogo.

      Mfalme wa kusini—chombo cha utawala kilichoongozwa na Zenobia—‘alijichochea’ afanye vita dhidi ya Aurelian “kwa jeshi kubwa mno na lenye nguvu nyingi” chini ya majenerali wawili, Zabdas na Zabbai. (Danieli 11:25b) Lakini Aurelian alitwaa Misri kisha akaanzisha safari ya uvumbuzi katika Asia Ndogo na Siria. Zenobia alishindiwa huko Emesa (sasa ni Homs), naye akakimbia kurudi Palmyra.

      Aurelian alipolizingira Palmyra, Zenobia akitumaini kupata msaada, alitoroka na mwana wake kuelekea Uajemi, lakini alishikwa na Waroma kwenye Mto Frati. Wapalmyra walisalimisha jiji lao katika 272 W.K. Aurelian aliwatendea wakazi wa hapo kwa ukarimu, akapora vitu vingi sana, kutia ndani sanamu iliyokuwa katika Hekalu la Jua, na kuondoka kwenda Roma. Maliki Mroma hakumuua Zenobia, bali alimfanya awe kivutio kikuu katika mwandamano wake wa shangwe ya ushindi katika Roma mwaka wa 274 W.K. Huko alibaki akiwa mwanamke mkomavu mwenye daraja la kuheshimiwa wa Roma katika maisha yake yote.

      Jiji la Jangwani Laharibiwa

      Miezi kadhaa baada ya Aurelian kutwaa Palmyra, Wapalmyra waliwaua askari walinzi wa Roma ambao alikuwa amewaacha. Habari ya uasi huu ilipofikia Aurelian, mara moja Aurelian aliamuru askari wake warudi huko tena, na wakati huu walilipiza kisasi kwa kiwango kikubwa dhidi ya wakazi wote wa huko. Wale walionusurika kutokana na machinjo hayo yasiyo na huruma walipelekwa utumwani. Jiji hilo lenye fahari liliporwa na kuharibiwa kiasi cha kwamba halingeweza kurekebishwa. Hivyo, jiji hilo kubwa lenye shughuli nyingi lilirudia tena hali yake ya zamani—“Tadmori wa nyikani.”

      Wakati Zenobia alipojasiria kukabili Roma, pasipo kujua yeye na Maliki Aurelian walitimiza mafungu yao wakiwa “mfalme wa kusini” na “mfalme wa kaskazini,” wakitimiza sehemu ya unabii uliorekodiwa kwa kina zaidi na nabii wa Yehova miaka 800 hivi mapema. (Danieli, sura ya 11) Akiwa mwenye utu wake wenye kutokeza, Zenobia alipendwa na watu wengi. Hata hivyo, la maana zaidi, lilikuwa fungu lake katika kuwakilisha chombo cha kisiasa kilichotabiriwa katika unabii wa Danieli. Utawala wake haukudumu kwa zaidi ya miaka mitano. Palmyra, jiji kuu la ufalme wa Zenobia, leo ni kijiji tu. Hata Milki yenye uwezo ya Roma tangu wakati huo imefifia na kuziachia nafasi falme za kisasa. Wakati ujao wa mamlaka hizi utakuwaje? Hali yao ya baadaye pia inaamuliwa na utimizo wa unabii wa Biblia.—Danieli 2:44.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki