Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Mfalme wa Kaskazini” Katika Wakati wa Mwisho
    Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2020 | Mei
    • 10. Andiko la Danieli 11:25b, 26 lilitimizwaje?

      10 Kisha Danieli anatabiri kuhusu kile kitakachoipata Milki ya Ujerumani na jeshi lake. Unabii huo unasema kwamba mfalme wa kaskazini “hatasimama.” Kwa nini? “Kwa sababu watapanga njama dhidi yake. Na wale wanaokula vyakula vyake bora watasababisha aanguke.” (Dan. 11:25b, 26a) Katika siku za Danieli, wale waliokula “vyakula bora ambavyo [mfalme] mwenyewe alikula” walitia ndani maofisa wa mfalme ‘waliomtumikia mfalme.’ (Dan. 1:5) Unabii huo unazungumza kuhusu nani? Unawahusu maofisa wa vyeo vya juu wa Milki ya Ujerumani—kutia ndani majenerali na washauri wa mambo ya kijeshi wa maliki—ambao hatimaye walipindua utawala wa maliki wa Ujerumani.e Unabii wa Danieli haukutabiri tu kuhusu kuanguka kwa milki hiyo, bali pia unataja matokeo ya vita kati ya mfalme wa kaskazini na wa kusini. Unabii huo unasema hivi kuhusu mfalme wa kaskazini: “Na jeshi lake litafagiliwa mbali, na wengi watauawa.” (Dan. 11:26b) Kama ilivyotabiriwa, jeshi la Ujerumani ‘lilifagiliwa mbali’ katika Vita vya Kwanza vya Ulimwengu, na watu wengi ‘waliuawa.’ Watu wengi sana walikufa katika vita hivyo kuliko vita vingine vyovyote kabla ya hapo.

  • “Mfalme wa Kaskazini” Katika Wakati wa Mwisho
    Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2020 | Mei
    • e Walifanya mambo mengi yaliyosababisha milki yao ianguke haraka. Kwa mfano, waliacha kumsaidia maliki, walivujisha siri kuhusu habari nyeti za vita, na kumlazimisha maliki ajiuzulu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki