-
Ufalme Umesimamishwa!Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2022 | Julai
-
-
10. (a) Muungano wa Uingereza na Marekani unatimizaje kwa usahihi unabii wa Danieli? (b) Tunapaswa kuepuka hatari gani? (Tazama sanduku “Jihadhari na Udongo wa Mfinyanzi!”)
10 Kwanza, tofauti na serikali kuu za ulimwengu zilizotajwa mwanzoni katika maono hayo, muungano wa Uingereza na Marekani hauwakilishwi na chuma tu kama vile dhahabu au fedha, bali ni mchanganyiko wa chuma na udongo wa mfinyanzi. Udongo wa mfinyanzi unafananisha “uzao wa wanadamu,” au watu wa kawaida. (Dan. 2:43, maelezo ya chini) Kama inavyoonekana wazi leo, maamuzi yao wakati wa uchaguzi, harakati zao za kutetea haki za kiraia, maandamano makubwa, na vyama vyao vya wafanyakazi, hudhoofisha uwezo wa serikali hiyo kuu ya ulimwengu kutekeleza sera zake.
-