Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kitabu Cha Biblia Namba 31—Obadia
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
    • 5. (a) Ni nini kinachotoa uthibitisho wa kwamba maandishi ya Obadia ni asilia na kweli? (b) Obadia alitimizaje matakwa ya nabii wa kweli, na kwa nini jina lake lafaa?

      5 Unabii wa Obadia juu ya Edomu ulitimizwa—wote! Katika kufikia upeo wao, unabii huo waeleza hivi: “Nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa BWANA [Yehova, NW] amesema hayo.” (Mst. 18) Edomu iliishi kwa upanga na ilikufa kwa upanga, na hakuna kidalili chochote cha kubakia kwa wazao wayo. Hivyo maandishi hayo yathibitishwa kuwa ni asilia na kweli. Obadia alikuwa na sifa zote za nabii wa kweli: Yeye alinena kwa jina la Yehova, unabii wake uliheshimu Yehova, na ulitimia kama vile ilivyothibitishwa na historia iliyofuata. Jina lake kwa kufaa lamaanisha “Mtumishi wa Yehova.”

  • Kitabu Cha Biblia Namba 31—Obadia
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
    • 12 Kulingana na Yosefo, katika karne ya pili K.W.K. Waedomi waliosalia walitiishwa na mfalme Myahudi John Hirkano 1, wakalazimishwa kukubali tohara, na polepole wakafyonzwa ndani ya utawala wa Kiyahudi chini ya liwali wa Kiyahudi. Kufuatia uharibifu wa Kiroma wa Yerusalemu katika 70 W.K., jina lao lilitokomea kutoka kwa historia.c Ilikuwa sawa na alivyokuwa ametabiri Obadia: “Utakatiliwa mbali hata milele. . . . Wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau.”—Oba. 10, 18.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki