Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maonyo ya Kimungu Yanayokuathiri Wewe
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Aprili 15
    • Mungu analeta afa juu ya wale walio na hatia ya kutenda jeuri dhidi ya watu wake. Ni nini sababu ya afa la Waedomi? Ni kurudia-rudia vitendo vya jeuri dhidi ya wana wa Yakobo, ndugu zao. Wakiwa wazao wa Esau, Waedomi walikuwa wa ukoo mmoja na Waisraeli. Hata hivyo, wanashtakiwa kuwateka nyara watu wenye ujamaa wao, wakishangilia kikorofi juu ya anguko la Yerusalemu, na kufikia upeo kwa kuwatia waokokaji katika mikono ya adui. Hivyo, Edomu imejitilia muhuri wa kuangamizwa kwayo.​—Mistari ya 10-16.

  • Maonyo ya Kimungu Yanayokuathiri Wewe
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Aprili 15
    • ○ Mstari 10​—Edomu ilihukumiwa maangamizi ‘kukatiliwa mbali hata milele’ kwa sababu ya chuki yayo yenye kusimanga na kutojali kabisa shauku ya kiasili kwa taifa ndugu yayo, “wana wa Yuda.” (Mstari 12) Kutoweka huko kwa taifa kulimaanisha kwamba taifa la Kiedomi lenye serikali na idadi ya watu katika mahali hususa pa kijiografia lingetoweka kabisa usoni pa dunia. Leo, hakuna watu wanaotambulikana kuwa wenye utaifa wa Kiedomi; wao ‘wamekuwa kana kwamba hawakuwa kamwe.’​—Mstari 16.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki