-
Maonyo ya Kimungu Yanayokuathiri WeweMnara wa Mlinzi—1989 | Aprili 15
-
-
Watumishi wa Mungu wanaweza kuwa na uhakika kwamba yeye atajibu sala zao. Akiwa ndani ya samaki, Yona anamlilia Yehova kuomba msaada, kwa sala anamshukuru Mungu kwa kumkomboa kutoka kaburi la maji, na kuahidi kulipa alichonadhiri. Baada ya muda, anatapikwa nje katika bara.—2:1-10.
-
-
Maonyo ya Kimungu Yanayokuathiri WeweMnara wa Mlinzi—1989 | Aprili 15
-
-
○ 2:1, 2—Kwa uhakika Yona hakuwa na hali nzuri kabisa za kuweza kutunga shairi alipokuwa “katika tumbo la yule samaki.” Lakini baadaye aliandika yaliyompata. Katika kina cha moyo wake mlitoka maneno yaliyoeleza maoni yake ya ndani ambayo yanalingana na yale yaliyo katika Zaburi. —Linganisha 2:2 pamoja na Zaburi 120:1 na Zab 130:1; Yon 2:5 pamoja na Zaburi 69:1.
-