Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Milki Iliyopotea Ambayo Iliwaaibisha Wahakiki wa Biblia
    Mnara wa Mlinzi—1993 | Juni 1
    • MWANAHISTORIA Mgiriki Diodorus Siculus aliishi miaka 2,000 iliyopita. Alidai kwamba Ninawi lilikuwa jiji lenye pande nne; zile pande nne zilikuwa na urefu wa ujumla wa stadia (kimo cha Kiroma cha kale) 480. Huo ni mduara wa kilometa 96! Biblia hutoa masimulizi ayo hayo, ikisimulia Ninawi kuwa jiji kubwa “mwendo wa siku tatu.”—Yona 3:3.

      Wahakiki wa Biblia wa karne ya 19 walikataa kuamini kwamba jiji lisilojulikana la ulimwengu wa kale lingaliweza kuwa kubwa jinsi hiyo. Walisema pia kwamba ikiwa Ninawi lilipata kuwako wakati wowote, ni lazima iwe lilikuwa sehemu ya ustaarabu wa kale uliotangulia Babuloni.

  • Milki Iliyopotea Ambayo Iliwaaibisha Wahakiki wa Biblia
    Mnara wa Mlinzi—1993 | Juni 1
    • Wakati uo huo, mwakiolojia mwingine, Austen Henry Layard, alianza kuyachimba mabomoko kwenye mahali paitwapo Nimrud karibu kilometa 42 kusini-magharibi mwa Khorsabad. Mabomoko hayo yalithibitika kuwa Kala—mojawapo yale majiji manne ya Kiashuru yanayotajwa kwenye Mwanzo 10:11. Halafu, katika 1849, Layard alifukua mabomoko ya jumba kubwa mno ya kifalme kwenye mahali paitwapo Kuyunjik, kati ya Kala na Khorsabad. Jumba hilo la kifalme lilithibitika kuwa sehemu ya Ninawi. Kati ya Khorsabad na Kala kuna mabomoko ya makao mengine, kutia na rundo liitwalo Karamles. “Tukichukua marundo hayo makubwa manne ya Nimrúd [Kala], Koyunjik [Ninawi], Khorsabad, na Karamles, yakiwa kona za mraba,” akaonelea Layard, “itaonekana kwamba pande zalo nne zinalingana kiasi fulani kwa usahihi na zile stadia 480 au maili 60 za yule mwanajiografia, zinazofanyiza ule mwendo wa siku tatu wa nabii [Yona].”

      Basi yaonekana, Yona alitia ndani makao hayo yote kuwa ‘jiji kubwa,’ moja akiyaita kwa jina la lile jiji linalotajwa kwanza kwenye Mwanzo 10:11, yaani, Ninawi. Ndivyo ifanywavyo leo. Kwa kielelezo, kuna tofauti kati ya lile jiji la awali la London na maeneo yalo ya mashambani, ambayo hufanyiza lile linaloitwa nyakati nyingine “London Kubwa Zaidi.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki