-
Jitahidi Kuwaona Wengine Kama Yehova AnavyowaonaMnara wa Mlinzi—2003 | Machi 15
-
-
5. Yona alipewa mgawo gani, naye alifanya nini?
5 Yona alikuwa nabii katika ufalme wa kaskazini wa Israeli katika siku za Mfalme Yeroboamu wa Pili, mwana wa Yoashi. (2 Wafalme 14:23-25) Siku moja, Yehova alimwagiza Yona aondoke Israeli na kusafiri kwenda Ninawi, mji mkuu wa Milki ya Ashuru yenye nguvu. Alipewa mgawo gani? Akawaonye Waninawi kwamba mji wao mkubwa ungeharibiwa. (Yona 1:1, 2) Badala ya kufuata maagizo ya Mungu, Yona alitoroka! Akapanda meli iliyokuwa inasafiri kwenda Tarshishi, mbali sana na Ninawi.—Yona 1:3.
-
-
Jitahidi Kuwaona Wengine Kama Yehova AnavyowaonaMnara wa Mlinzi—2003 | Machi 15
-
-
9. Yona alionyesha sifa gani tufani kubwa ilipotisha mabaharia?
9 Yona hakutaka kutii agizo la Yehova, hivyo akapanda meli iliyompeleka mbali sana na mahali alipotumwa. Hata hivyo, Yehova hakumwacha wala kutuma nabii mwingine badala ya Yona, bali alijaribu kumsaidia aone umuhimu wa mgawo wake. Mungu alisababisha tufani kubwa baharini. Meli iliyombeba Yona ilipeperushwa huku na huko na mawimbi. Watu wasio na hatia walikuwa karibu kuangamia kwa sababu ya Yona! (Yona 1:4) Yona angefanyaje? Kwa kuwa hakutaka mabaharia waliokuwa katika meli hiyo waangamie kwa sababu yake, Yona aliwaambia hivi: “Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itatulia.” (Yona 1:12) Hatimaye, mabaharia walipomtupa baharini, Yona hangetarajia Yehova amwokoe. (Yona 1:15) Hata hivyo, Yona alikuwa tayari kufa ili mabaharia hao wasiangamie. Kwa kufanya hivyo, yeye alionyesha kwamba alikuwa na ujasiri, unyenyekevu, na upendo.
-