-
Haki na Jina la Yehova VyakwezwaMnara wa Mlinzi—1989 | Mei 1
-
-
Yehova anatarajia haki izoewe na wale wanaochukua daraka miongoni mwa watu wake. Kwa viongozi wa Israeli wanaotumia daraka vibaya, inasemwa hivi: “Je! haiwapasi ninyi kujua hukumu [haki, NW]? ninyi mnaoyachukia mema, na kuyapenda mabaya; ninyi mnaowachuna watu ngozi yao, na nyama mifupani mwao.” Akiwa na ‘roho ya Yehova, ya hukumu [haki, NW] na uwezo,’ Mika anatangaza hukumu za Mungu dhidi yao. Anasema kwamba viongozi hao wasio na haki wanahukumu ili kupata mahongo, makuhani wanaagiza ili kupata bei, na wanabii wanazoea uaguzi ili kupata pesa. Kwa hiyo, Yerusalemu “utakuwa magofu” tu.—3:1-12.
-
-
Haki na Jina la Yehova VyakwezwaMnara wa Mlinzi—1989 | Mei 1
-
-
○ 3:1-3—Huu ni utofautisho wa kugutusha kati ya Yehova, aliye Mchungaji mwenye fadhili, na viongozi wakatili wa watu wake wa kale katika siku ya Mika. Walishindwa kufanya utume wao wa kulinda kundi la kondoo kwa kujizoeza haki. Walinyonya kondoo wa kitamathali kwa ukatili si kwa kuwanyoa tu bali pia kwa ‘kuwachuna ngozi’—kama majibwa-mwitu. Hao wachungaji waovu walinyima watu haki, wakiwatiisha kwenye “vitendo vya umwagaji wa damu.” (3:10, NW) Kupitia hukumu zilizopotoshwa, wasio na kinga walipunjwa nyumba na riziki zao.—2:2; linganisha Ezekieli 34:1-5.
-