Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tutatembea Katika Jina la Yehova Milele!
    Mnara wa Mlinzi—2003 | Agosti 15
    • 15. Unaweza kuelezaje kwa maneno yako mwenyewe unabii wa Mika 4:1-4?

      15 Tunapofikiria unabii huo, tunaona kwamba sasa Mika anatoa ujumbe wa tumaini wenye kusisimua. Tunapata maneno yenye kutia moyo kama nini katika Mika 4:1-4! Mika anasema: “Itakuwa katika siku za mwisho ya kwamba mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi. . . . Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea [‘atayanyoosha mambo kuhusu,’ NW] mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha BWANA wa majeshi kimesema hivi.”

  • Tutatembea Katika Jina la Yehova Milele!
    Mnara wa Mlinzi—2003 | Agosti 15
    • 17 Kupatana na unabii wa Mika, hivi karibuni watu wote duniani watafuata kikamili ibada safi ya Yehova. Leo, watu ‘walio na mwelekeo ufaao kwa ajili ya uhai udumuo milele’ wanafundishwa njia za Yehova. (Matendo 13:48) Yehova anafanya hukumu na kunyoosha mambo kiroho kwa waamini wanaounga mkono Ufalme. Wataokoka “dhiki kubwa” wakiwa sehemu ya “umati mkubwa.” (Ufunuo 7:9, 14) Kwa kuwa wamefua panga zao kuwa majembe, hata leo watu hao wanaishi kwa amani pamoja na Mashahidi wenzao na watu wengine. Inafurahisha kama nini kuwa kati yao!

      Kuazimia Kutembea Katika Jina la Yehova

      18. ‘Kuketi chini ya mzabibu na mtini wako’ humaanisha nini?

      18 Tunasisimuka kuona wengi wakijifunza njia za Yehova wakati huu ambapo watu duniani pote wanaogopa sana. Tunatamani sana wakati ambapo hivi karibuni watu wote wanaompenda Mungu hawatajifunza vita tena bali wataketi chini ya mzabibu na mtini wao. Mara nyingi mitini hupandwa katika mashamba ya mizabibu. (Luka 13:6) Kuketi chini ya mzabibu na mtini wako humaanisha kuwa na amani, ufanisi, na usalama. Hata sasa, uhusiano wetu pamoja na Yehova hutupatia amani ya akili na usalama wa kiroho. Hali hizo zitakapokuwako chini ya utawala wa Ufalme, hatutaogopa chochote, tutakuwa salama salimini.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki