-
Alikata “Kauli Moyoni Mwake”Mnara wa Mlinzi—2008 | Oktoba 1
-
-
Safari ya Kwenda Bethlehemu
Si Yosefu na Maria peke yao waliokuwa wakisafiri. Kaisari Augusto alikuwa ametoa amri kwamba watu wote katika nchi waandikishwe na watu walihitaji kusafiri hadi kwenye mji waliozaliwa ili waandikishwe. Yosefu alifanya nini? Simulizi hilo linasema: “Yosefu pia akapanda kutoka Galilaya, kutoka jiji la Nazareti, akaingia Yudea, kwenye jiji la Daudi, linaloitwa Bethlehemu, kwa sababu alikuwa mshiriki wa nyumba na familia ya Daudi.”—Luka 2:1-4.
Halikuwa jambo lisilotarajiwa kwamba Kaisari alitoa amri yake wakati huo. Unabii ulioandikwa karne saba hivi mapema ulitabiri kwamba Masihi angezaliwa Bethlehemu. Kulikuwa na mji unaoitwa Bethlehemu kilomita 11 tu kutoka Nazareti. Hata hivyo, unabii ulitaja kihususa kwamba Masihi angetoka “Bethlehemu Efratha.” (Mika 5:2) Kijiji hicho kidogo kilicho upande wa kusini kiko umbali wa kilomita 150 hivi kutoka Nazareti ukitumia barabara za siku hizi za mlimani. Hiyo ndiyo Bethlehemu ambayo Yosefu aliamriwa aende kwani hilo ndilo lililokuwa chimbuko la ukoo wa Mfalme Daudi. Yosefu na mke wake walikuwa wa ukoo huo.
-
-
Alikata “Kauli Moyoni Mwake”Mnara wa Mlinzi—2008 | Oktoba 1
-
-
Ni nini kingine kilichomchochea Maria atii? Je, alijua unabii wa kwamba Masihi angezaliwa Bethlehemu? Biblia haisemi. Hatuwezi kupuuza uwezekano huo, kwa maana jambo hilo lilijulikana na viongozi wa kidini na watu kwa ujumla. (Mathayo 2:1-7; Yohana 7:40-42) Maria pia aliyajua Maandiko. (Luka 1:46-55) Vyovyote vile, iwe Maria alisafiri ili kumtii mumewe, kutii Kaisari, au kwa sababu ya unabii wa Yehova au iwe alichochewa na mambo hayo yote matatu, aliweka mfano bora. Yehova anathamini sana roho ya unyenyekevu na utii inayoonyeshwa na wanaume na wanawake. Siku hizi ambapo kujitiisha ni mojawapo ya sifa zinazodharauliwa, mfano wa Maria ni kielelezo kizuri kwa watu waaminifu kila mahali.
-