-
Wenye Shangwe Katika Mungu wa Wokovu WetuMnara wa Mlinzi—2000 | Februari 1
-
-
18. Ingawa Habakuki alitazamia magumu, alikuwa na mtazamo gani?
18 Nyakati zote vita hutokeza magumu, hata kwa wale wanaoibuka wakiwa washindi. Huenda chakula kikapungua. Huenda mali zikapotezwa. Huenda viwango vya maisha vikashuka. Iwapo hayo yatupata, tutatendaje? Habakuki alikuwa na mtazamo unaofaa kuigwa, kwani alisema hivi: “Maana mtini hautachanua maua, wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; taabu ya mzeituni itakuwa bure, na mashamba hayatatoa chakula; zizini hamtakuwa na kundi, wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe; walakini nitamfurahia BWANA nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.” (Habakuki 3:17, 18) Habakuki alitarajia magumu, huenda alitarajia njaa kuu. Hata hivyo, hakupoteza kamwe shangwe yake katika Yehova, aliye chanzo cha wokovu wake.
-
-
Wenye Shangwe Katika Mungu wa Wokovu WetuMnara wa Mlinzi—2000 | Februari 1
-
-
20. Japo magumu ya muda, twapaswa kuazimia kufanya nini?
20 Kwa hiyo, ijapokuwa magumu yoyote ya muda ambayo ni lazima tuyakabili, hatutapoteza imani katika nguvu ya kuokoa ya Yehova. Wengi wa ndugu na dada zetu katika Afrika, Ulaya Mashariki, na sehemu nyinginezo hulazimika kukabili magumu mazito, lakini wao hufuliza ‘kushangilia katika Yehova.’ Sisi nasi, kama wao, tusikome kamwe kufanya vivyo hivyo. Kumbuka Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova ndiye Chanzo cha ‘nguvu zetu.’ (Habakuki 3:19) Hawezi kututamausha kamwe. Har–Magedoni itakuja hakika, na pasipo shaka ulimwengu mpya ulioahidiwa na Mungu utafuata. (2 Petro 3:13) Kisha “dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa BWANA, kama maji yaifunikavyo bahari.” (Habakuki 2:14) Hadi wakati huo mzuri ajabu, na tufuate kielelezo kizuri cha Habakuki. Na sikuzote ‘tumfurahie Yehova na kumshangilia Mungu wa wokovu wetu.’
-