Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kitabu Cha Biblia Namba 35—Habakuki
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
    • 3. Ni hali gani zenye kuathiri Yuda zinazosaidia kuonyesha wakati wa uandikaji wa Habakuki?

      3 Ni wakati gani Habakuki alipofanya matangazo yake? Andishi lililotangulia kutajwa na maneno “BWANA [Yehova, NW] yumo ndani ya hekalu lake takatifu” yaonyesha kwamba hekalu katika Yerusalemu lilikuwa lingaliko. (2:20) Jambo hilo, pamoja na ujumbe wa unabii huo, ladokeza kwamba ulinenwa muda usio mrefu kabla ya uharibifu wa Yerusalemu katika 607 K.W.K. Lakini miaka mingapi kabla? Lazima iwe ilikuwa baada ya utawala wa Mfalme Yosia mcha-Mungu, 659-629 K.W.K. Unabii wenyewe watoa kidokezi katika kutabiri utendaji ambao watu katika Yuda hawataamini hata ukisimuliwa. Ni utendaji gani huo? Ni kuinuliwa kwa Wakaldayo (Wababuloni) na Mungu ili waadhibu Yuda isiyo na uaminifu. (1:5, 6) Hiyo ingelingana na sehemu ya mapema ya utawala wa Mfalme Yehoyakimu mwenye kuabudu sanamu, wakati ambapo kutokuamini na ukosefu wa haki ulikuwa umeenea mno katika Yuda. Yehoyakimu alikuwa amewekwa juu ya kiti cha ufalme na Farao Neko, na taifa lilikuwa chini ya uvutano wa Misri. Wakiwa chini ya hali hizo, watu wale wangehisi walikuwa na kisababishi cha kupuuza uwezekano wowote wa kuvamiwa na Babuloni. Lakini Nebukadreza alishinda Farao Neko katika pigano la Karkemishi katika 625 K.W.K., hivyo akivunja nguvu ya Misri. Kwa hiyo unabii huo ungalikuwa umetolewa kabla ya tukio hilo. Kwa hiyo vionyesho vyaelekeza kwenye mwanzo wa utawala wa Yehoyakimu (ulioanza katika 628 K.W.K.), hiyo ikifanya Habakuki awe mwenye kuishi wakati ule ule na Yeremia.

  • Kitabu Cha Biblia Namba 35—Habakuki
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
    • 6. Hali ni nini katika Yuda, na ni utendaji gani wa kustaajabisha ambao basi Yehova ataendesha?

      6 Nabii huyo amlilia Yehova (1:1–2:1). Ukosefu wa imani katika Yuda umeamsha maswali katika akili ya Habakuki. “Ee BWANA [Yehova, NW], nilie hata lini, wewe usitake kusikia?” yeye auliza. “Mbona wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi?” (1:2, 3) Sheria yafa ganzi, mwovu azingira mwadilifu, na haki yatokea ikiwa imepotoka. Kwa sababu hiyo, Yehova ataendesha utendaji ambao utasababisha ustaajabu, jambo ambalo watu hao ‘hawataliamini hata wakiambiwa.’ Kwa kweli yeye ‘anaondokesha Wakaldayo’! Yenye kuogofya kweli kweli ni njozi ambayo Yehova atoa juu ya hili taifa kali likija kasi sana. Limejitia bidii kutenda jeuri, na lakusanya watekwa “kama mchanga.” (1:5, 6, 9) Hakuna kitu kitakacholifungia njia, wala hata wafalme na maofisa wa daraja la juu, kwa maana lawacheka wote hao. Lateka kila mahali penye ngome. Yote hayo yatendeka ili yawe hukumu na karipio kutoka kwa Yehova, ‘Mtakatifu.’ (1:12) Habakuki angojea kwa usikivu Mungu anene.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki