-
Wokovu Unawezekana Mungu Alipizapo KisasiMnara wa Mlinzi—1989 | Mei 15
-
-
Yehova husikiliza maombi ya kusihi ya watumishi wake. Habakuki anauliza: “Ee BWANA, nilie hata lini, wewe usitake kusikia?” Ndiyo, hakuna haki, na waovu wanawazunguka waadilifu. Lakini Mungu anasikia, naye ‘anawaondokesha Wakaldayo’ wawe chombo chake cha kutolea adhabu. Hata hivyo, yeye anawezaje kutumia taifa kubwa la kivita? Mnabii anangoja jibu la Mungu, akitazamia karipio.—1:1—2:1.
-
-
Wokovu Unawezekana Mungu Alipizapo KisasiMnara wa Mlinzi—1989 | Mei 15
-
-
○ Habakuki 1:2-4—Imani ya Habakuki katika Yehova akiwa Mungu asiyevumilia uovu ilimharakisha kuuliza ni kwa nini uovu uliendelea kuwapo. Yeye alikuwa na nia ya kurekebishwa kufikiri kwake. (2:1) Wakati sisi tunaposhangaa ni kwa nini mambo fulani yanavumiliwa, uhakika wetu katika uadilifu wa Yehova unapasa kutusaidia sisi vilevile tuendeleze usawaziko wetu na kumngojea yeye.—Zaburi 42:5, 11.
-