Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Na Tuwe Namna Iliyo na Imani
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Desemba 15
    • 8. Kielelezo cha Habakuki kingeweza kuwasaidiaje Wakristo wa karne ya kwanza na wa leo?

      8 Habakuki hakujua jinsi uharibifu wa Yerusalemu ulivyokuwa umekaribia. Kwa njia iyo hiyo, Wakristo wa karne ya kwanza hawakujua wakati ambapo mfumo wa Kiyahudi ungefikia mwisho. Wala sisi leo hatujui “siku hiyo na saa hiyo” ambapo hukumu ya Yehova itatekelezwa dhidi ya mfumo huu mwovu. (Mathayo 24:36) Basi, ebu tuone jibu lenye sehemu mbili ambalo Yehova alimpa Habakuki. Kwanza, alimhakikishia nabii huyo kwamba mwisho ungefika kwa wakati barabara. ‘Hautakawia,’ Mungu akasema, hata ingawa wanadamu wanaweza kuona kwamba unakawia. (Habakuki 2:3) Pili, Yehova alimkumbusha Habakuki: “Lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.” (Habakuki 2:4) Hizo ni kweli nzuri na sahili kama nini! Jambo muhimu zaidi si mwisho utakuja lini, bali ni kama tutaendelea kuishi maisha yenye imani.

      9. Watumishi watiifu wa Yehova waliendeleaje kuishi kwa uaminifu (a) mwaka wa 607 K.W.K.? (b) baada ya mwaka wa 66 W.K.? (c) Kwa nini ni muhimu kwamba tuimarishe imani yetu?

      9 Yerusalemu lilipoporwa mwaka wa 607 K.W.K., Yeremia, na mwandishi wake Baruki, Ebed-meleki, na wale Warekabi waaminifu-washikamanifu waliona ukweli wa ahadi ambayo Yehova alimpa Habakuki. Wao ‘walipata kuishi’ kwa kuokoka uharibifu wenye kuhofisha wa Yerusalemu. Kwa nini? Yehova alithawabisha uaminifu wao. (Yeremia 35:1-19; 39:15-18; 43:4-7; 45:1-5) Vivyo hivyo, ni lazima Wakristo Waebrania wa karne ya kwanza wawe walitii shauri la Paulo, kwa sababu majeshi ya Waroma yaliposhambulia Yerusalemu mwaka wa 66 W.K. na kuondoka kwa sababu isiyoeleweka, Wakristo hao walitii kwa uaminifu onyo la Yesu la kutoroka. (Luka 21:20, 21) Wao waliendelea kuishi kwa sababu ya uaminifu wao. Vilevile, sisi tutaendelea kuishi tukipatikana tukiwa waaminifu mwisho ufikapo. Hiyo ni sababu nzuri kama nini ya kuimarisha imani yetu sasa!

  • Na Tuwe Namna Iliyo na Imani
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Desemba 15
    • a Paulo alinukuu tafsiri ya Septuagint ya Habakuki 2:4, ambayo imetia ndani maneno “ikiwa yeyote arudi nyuma, nafsi yangu haina upendezi katika yeye.” Taarifa hiyo haionekani katika hati-kunjo za Kiebrania zilizoko. Wengine wamedokeza kwamba Septuagint hiyo ilitegemea hati-kunjo za zamani za Kiebrania ambazo hazipo wakati huu. Hata hivyo, Paulo aliongozwa na roho ya Mungu kutumia maneno haya hapa. Kwa hiyo Mungu ameyakubali maneno hayo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki